Hatimae
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini, imetoa majina ya wanafunzi
ambao wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali kwa ajili ya kuendelea na
elimu ya sekondari kidato cha tano, sanjari na vyuo mwaka 2014.
Orodha hiyo
imetangazwa jijini Dar es salaam tarehe 17/06/2014, ambapo idadi ya wasichana
waliochaguliwa kwa nafasi hizo ni 9,378, waliochaguliwa katika machaguo 13 ya
masomo mbalimbali ya kidato cha tano na masomo 11 ya vyuo vya ufundi.
Shule
zilizopangiwa wanafunzi ni 201, ambapo shule za wasichana pekee ni 61, huku
shule 34 zikiwa za jinsia zote mbili, wasichana na wavulana.
Idadi ya
wanafunzi wavulana waliochaguliwa katika machaguo 13 ya masomo mbalimbali ya
ngazi hiyo, ni 22,138.
WASICHANA-SHULE-ZOTE
WAVULANA-MAJINA-YA-SHULE-A-mpaka-L
WAVULANA-MAJINA-YA-SHULE-M-mpaka-Z
Aidha Serikali ya
Tanzania imesema kuwa wanafunzi 16,800 wakiwemo watahiniwa wa kujitegemea 10,
wenye sifa lakini wamekosa nafasi za kujiunga kidato cha tano, sasa
wataanzishiwa utaratibu wa kusoma stashahada ya ualimu pamoja na kidato cha
tano na sita.
Utaratibu
huo mpya ulitangazwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa, wakati akitangaza
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na ualimu jana June 17, 2014.
Kwa mujibu
wa Majaliwa, zimeteuliwa shule maalumu ambapo wanafunzi hao watapatiwa mafunzo
hayo ya kidato cha tano, sita na stashahada ya ualimu kwa pamoja.
Akitangaza
waliochaguliwa, alisema kuwa jumla ya wanafunzi 54,085 sawa na asilimia 75 ya
wanafunzi 71,527 waliostahili kuingia kidato cha tano Tanzania Bara kwa mwaka
huu, wamechaguliwa.
Kati yao,
wavulana 14,826 sawa na asilimia 27 watasoma sanyansi na 16,526 sawa na
asilimia 14, watasoma sayansi ya jamii.
Katika
orodha hiyo, wamo wasichana 7,859 sawa na asilimia 14 ambao watasoma sayansi na
14,874 sawa na asilimia 27 watasoma sayansi ya jamii.
Majaliwa
alisema wanafunzi hao watajiunga kidato cha tano katika shule 241 zikiwemo 33
ambazo zimepangiwa wanafunzi kwa mara ya kwanza.
Jumla ya
wanafunzi wapatao 235,227 wa kidato cha nne mwaka 2013 sawa na asilimia 58.21
ya watahiniwa wote wamefaulu kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo
mbalimbali vya serikali, matokeo hayo yanaonesha kiwango cha ufaulu kimepanda
kwa asilimia 15.13.
No comments:
Post a Comment