UCHAGUZI MKUU 2015-TANZANIA:- Dk Wilbrod Slaa asema’’Sina Mpango wa Kugombea Urais 2015 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 11, 2014

UCHAGUZI MKUU 2015-TANZANIA:- Dk Wilbrod Slaa asema’’Sina Mpango wa Kugombea Urais 2015 .



Katibu Mkuu wa CHADEMA; Dk Wilbrod Slaa.

DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa katika kundi la UKAWA.

Kila kitu kitafanywa kwa wakati muafaka,kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.

Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, ninaheshimu uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.

UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala la rais,serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.

Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba."

Chanzo:-Mtanzania Juni 11-2014

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad