Vipaumbele
vya Bajeti hiyo, kwa maana ya miradi itakayozingatiwa zaidi, ni iliyo katika
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaohusisha sekta sita za Kilimo, Elimu,
Maji, Utafutaji rasilimali fedha, Nishati, Uchukuzi na Uboreshaji wa Mazingira
ya kufanyia biashara na Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano.
Kwa upande
wa Kenya, hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Kenya, itasomwa na Waziri wa Fedha,
Henry Rotich.
Katika
taarifa yake kwa wabunge wa Kenya mwezi Machi mwaka huu, Rotich alieleza kuwa
Bajeti ya Kenya kwa mwaka wa Fedha wa 2014/15, itakuwa Shilingi za Kenya
Trilioni 1.8.
Waziri wa
Fedha wa Uganda, Maria Kiwanuka ndiye atakayesoma hotuba ya Bajeti ya Serikali
ya Uganda kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Wazir Kiwanuka
ataeleza hatua mbalimbali za kuinua uchumi, kupunguza kodi mbalimbali na
kudhibiti mfumko wa bei.
Hivi
karibuni, Kiwanuka alikaririwa akisema kuwa uchumi wa Uganda unaendelea kukua
kwa kasi, lakini siyo katika viwango vya miaka 1990 na 2000, ambapo ulikua kwa
asilimia 7.
Kwa upande
wa Rwanda, hotuba ya Bajeti ya Serikali itasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango
ya Uchumi wa Rwanda, Claver Gatete.
Bajeti yote
ya Rwanda kwa mwaka 2014/15 inatarajia kuwa Faranga za Rwanda bilioni 1,753.
Kwa mujibu
wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), uchumi wa Rwanda unatarajia kukua kwa
asilimia 6 katika mwaka wa fedha 2014/15, ukilinganisha na asilimia 4.6 mwaka
2013.
Waziri
wa Fedha, Mipango ya Uchumi na Maendeleo wa Burundi, Tabu Abdallah Manirakiza,
ndiye atasoma bajeti ya Serikali ya Burundi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Tayari
Shirika la Fedha Duniani (IMF) limekadiria kuwa uchumi wa Burundi, utakua kwa
asilimia 7 katika mwaka 2014/15, ukilinganisha na asilimia 4.5 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment