KUNYWA SUMU:-Ataka kujiua kwa wivu wa Kimapenzi,wilayani Ngara...'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 02, 2014

KUNYWA SUMU:-Ataka kujiua kwa wivu wa Kimapenzi,wilayani Ngara...''

Jeshi la Polisi wilayani Ngara  mkoani Kagera  linamshikilia msichana  mwenye umri wa miaka 18  mkazi  wa  Musoma mkoani Mara  kwa  tuhuma za kutaka kujiua kwa kunywa sumu kutokana na wivu wa kimapenzi baina yake na Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Ntobeye wilayani Ngara..Picha Na:-Maktaba.
Msichana huyo Rosemary Marwa  mkazi wa Musoma ambaye awali alijitambulisha kuwa ni mkazi wa Dar es salaam, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Murgwanza tangu May 28 mwaka huu ,akipatiwa matibabu na ameruhusiwa May 31,mwaka huu  baada ya kupon.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara ,Bw Abeli Mtagwa amesema kwa sasa msichana huyo bado anahojiwa na polisi na kwamba anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho (June 03,2014) baada ya upelelezi kukamilika ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo Bw Mtagwa amekemea tabia ya watu kutaka kujiua kwa kisingio cha wivu wa Kimapenzi na Ugumu wa Maisha na kwamba serikali itaendelea kuwachukulia hatua wote watakaobainika kufanya hivyo.

Habari Na:-Radio Kwizera FM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad