PICHA / TUZO ZA WATU TANZANIA 2014:-Angalia walioshinda Tanzania People’s Choice Awards 2014 katika sherehe zilizofanyika June 27,2014 jijini Dar Es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 29, 2014

PICHA / TUZO ZA WATU TANZANIA 2014:-Angalia walioshinda Tanzania People’s Choice Awards 2014 katika sherehe zilizofanyika June 27,2014 jijini Dar Es Salaam.

Tuzo za watu zimefanyika usiku wa tarehe 27,June 2014, kwenye hotel ya Serena Hotel.
Baadhi ya tuzo zilienda kama hivi, Muigizaji wa kike anayependwa-Elizabeth Michael, Mwigizaji wa kiume anayependwa – Mzee Majuto,Video ya muziki ya muimbaji wa kiume imeenda kwa Diamond Platinumz (My number 1),Lady Jay Dee ameshinda tuzo ya video inayopendwa ya muimbaji wa kike na video ya Yahaya. Tuzo ya mtangazaji wa radio anayependwa ni Millard Ayo na show ya radio inayopendwa ni Amplifaya.

Filamu inayopendwa imeenda kwa Ndoa yangu, Juma Kaseja akishinda mwanamichezo anayependwa, Nisher ameshinda ya muongozaji wa video anayependwa,Salim Kikeke ameshinda ya mtangazaji wa TV anayependwa, Salama Jabil ameshinda ya mtangazaji wa TV wa kike anayependwa na nyingine ziliendelea.

Mkongwe King Majuto (kulia) akiwapa mashabiki wake heko kwa kumpigia kura. Ameshinda kipengele cha Muigizaji wa Kiume Anayependwa Kwenye Filamu.
Picha ya pamoja ya walionufaika katika Tuzo za Watu mjini Dar Es Salaam, Juni 27, 2014.
Picha ya pamoja huku wa pili kushoto ni  Lulu Michael, mshindi wa Mwigizaji wa Kike Kwenye Filamu Anayependwa.
MC Jimmy Kabwe akiwa kazini – Tuzo za Watu 2014...

Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.

ORODHA YA WASHINDI WA TUZO HIZO.

1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA

Millard Ayo – Clouds FM

2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA

Amplifaya – Clouds FM

3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA

Salim Kikeke – BBC Swahili

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA

Mkasi – EATV

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA

Juma Kaseja – Yanga

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA

Nisher

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME

My Number One – Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE

Yahaya – Lady Jaydee

09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA

King Majuto

10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA

Elizabeth ‘Lulu’ Michael

11. FILAMU INAYOPENDWA

Ndoa Yangu

Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lynn
Faraja Nyalandu
Jacqueline Wolper naye alikuwepo katika Tuzo hizo za Watu 2014 zilizofanyika Usiku wa June 27,2014.
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
Kichwa chenyewe ndiyo hiki, Luca Neghesti mwasisi wa Tuzo za Watu. Kijana ana mipango mizuri, anastahili kuungwa mkono. Boss wa Bongo5 pia.
Hamza Kasongo, mkongwe katika fani ya utangazaji Tanzania akimkabidhi Tuzo Salim Kikeke.
Mtangazaji maarufu Salim Kikeke wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza la Tuzo za Watu za Tanzania 2014 au Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika Serena Hotelhttp://cdncache-a.akamaihd.net/items/it/img/arrow-10x10.png, Ijumaa June 27,2014 jijini Dar Es Salaam.
JB akimkabidhi Elizabert Michael aka Lulu tuzo ya Mwigizaji wa Filamu wa Kike Anayependwa.
Salim Kikeke (katikati), Mtangazaji wa Runinga Anayependwa akiwa na Luca Neghesti na Nancy Sumari waandalizi wa Tuzo za Watu 2014.

Sasa hapa Majuto (kofia nyeupe) huwezi kujua anaigiza au la! Lakini huyu kweli mkongwe, toka enzi za DDC Magomeni Kondoa, chuma kimedumu sana hiki. Jacqueline Wolper yuko na simu, sijui ni Instagram au…!?

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad