KOMBE LA DUNIA 2014:-Tazama Picha Yaliyojiri wakati Brazil wakitinga Robo fainali huku Chile ikifa kiume kwa kutolewa kwa Penati 3-2-June 28,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 29, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Tazama Picha Yaliyojiri wakati Brazil wakitinga Robo fainali huku Chile ikifa kiume kwa kutolewa kwa Penati 3-2-June 28,2014.

Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2014, Brazil wameitoa Chile kwa penalti 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia huko Estádio Governador Magalhães Pinto, Jijini Belo Horizonte,June 28,2014, baada kutoka Sare 1-1 katika Dakika 90 na pia kumalizika nyongeza ya Dakika 30 bila Mshindi na hatimae Brazil kupita kwa Mikwaju ya Penati  huku Kipa wao Julio Cesar akiibuka Shujaa kwa kuokoa Penati 2 kati ya hizo.

Brazil walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 18 la David Luiz alieunganisha Mpira uliopigwa Kona na Neymar na kugongwa na Thiago Silva.



Chile walisawazisha kwenye Dakika ya 32 kwa Bao la Alexis Sanchez huku kipindi cha Pili Hulk aliifungia Brazil Bao la Pili lakini Msaidizi wa Refa Howard Webb aliashiria Mbrazil huyo alishika kabla kufunga.





Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilikuwa 1-1 na Nyongeza ya Dakika 30 haikuzaa Mshindi na Mechi kuingia Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Brazil walishinda kwa Penati 3-2 na kutinga Robo Fainali ambapo watakutana na Colombia aliyemtoa Uruguay kwa kumfunga bao 2-0.

MIKWAJU YA PENATI 5.

Brazil 3 Chile 2

Brazil 1-0 Chile
  
-David Luiz alifunga

Brazil 1-0 Chile

-Mauricio Pinilla alikosa, Kipa Julio Cesar aliokoa

Brazil 1-0 Chile

-Willian alikosa, alipiga nje!

Brazil 1-0 Chile

-Alexis Sanchez alikosa, Kipa Julio Cesar aliokoa

Brazil 2-0 Chile

-Marcelo alifunga

Brazil 2-1 Chile

-Hulk alikosa, Kipa Bravo aliokoa

Brazil 2-1 Chile

-Charles Aranguiz alifunga

Brazil 2-2 Chile

-Marcelo Diaz alifunga

Brazil 3-2 Chile

-Neymar alifunga

Brazil 3-2 Chile

-Gonzalo Jara alikosa

SHUJAA NI KIPA WA BRAZIL, JULIO CESAR, KWA KUOKOA PENATI 3.




KOMBE LA DUNIA
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
**Saa za Bongo.

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil 1 - 1  Chile - Penati 3-2
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia 2 - 0 Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador







ROBO FAINALI -IJUMAA, JULAI 4, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Mshindi 53 v Mshindi 54 [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

2300
Brazil v Mshindi 50 [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza

JUMAMOSI, JULAI 5, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Mshindi 55 v Mshindi 56 [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia

2300
Mshindi 51 v Mshindi 52 [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador


NUSU FAINALI -JUMANNE, JULAI 8, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte

JUMATANO, JULAI 9, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 59 Mshindi 60 [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo


MSHINDI WA TATU -JUMAMOSI, JULAI 12, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia


FAINALI-JUMAPILI, JULAI 13, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad