Alysia
Montano, mwenye mimba ya wiki 34 akishindana katika mbio za mita 800 za US
Track na Field Championships.
|
Mama Mjamzito Alysia Montano amekimbia mbio za mita 800 za US Track na Field
Championships jana (June 26,20140, ingawa mimba yake imetimiza wiki 34.
Bingwa huyo
mara tano wa taifa alitumia muda wa dakika mbili na sekunde, 32.13 kumaliza na
kufuzu hatua nyingine, akiwa amebakiza wiki saba tu kabla ya kujifungua.
Mwanamke
huyo mwenye umri wa miaka 28, nyota wa zamani Chuo Kikuu cha California,
kumaliza wa mwisho haikumuumiza mbele ya umati waliojitokeza kushuhudia mbio hizo kwenye Uwanja wa Hornet.
Alianza kwa
kasi na kuongoza kwa umbali wa mita 120 kabla ya kuanza kuishiwa nguvu na
kupatwa.
Montano
akiwa kwenye mashindano mjini Sacramento.
|
Montano
akisubiri mbio kuanza katika siku ya ufunguzi wa USATF Outdoor Championship..Habari
Na:-Bin Zuber.
|
No comments:
Post a Comment