PICHA:-Tazama Taswira ya Barabara mpya ya kuelekea Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ngara ambayo awali iliokuwa imefungwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 03, 2014

PICHA:-Tazama Taswira ya Barabara mpya ya kuelekea Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ngara ambayo awali iliokuwa imefungwa.

Kufunguliwa kwa barabara hiyo hivi sasa ni Historia na kumbukumbu muhimu sana kwa Wakazi wa Ngara na hata kwa Mkuu wa wilaya wa sasa wa Ngara Bw.Costantine Kanyasu,kwani hapo awali ilifungwa kwa kuwekewa Vigingi isipitike au isitumike na wananchi na kiongozi mmojawapo aliyewahi kuwa pia mkuu wa wilaya hiyo.



Awali daraja hilo lilifungwa kwa kuwekwa Vigingi ambavyo vilifanya magari kutopitia na kuwa kama uchochoro wa kupita watu pekee waliokuwa wakienda kupata huduma za kiofisi katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ,Idara ya Elimu shule za Msingi wilaya,Idara ya Kilimo ya wilaya na Hata Mahakama ya Wilaya ya Ngara na Kituo cha Polisi.



Barabara hiyo sasa imekuwa na mvuto pia baada ya miti iliyokuwa imetanda kama kichaka kukatwa vizuri na kufanya muonekano wake uwe wa kupendeza kama picha zinavyokuonesha.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad