![]() |
Kikosi cha Bandari Biharamulo kilichofungwa bao 1-0 na Ngara Stars kwenye mchezo wa kuwania Mazagazaga Cup 2014.
|
![]() |
Muonekano wa uwanja wa Shule ya Msingi Nyakanazi unaotumiwa kushindana timu kuwania Kombe la Mazagazaga 2014 ,likiwa na thamani ya shilingi Laki 8 kwa mshindi wa Kwanza atakayelinyakuwa.
|
![]() |
Mfungaji wa goli la Ngara Stars Wise Khalifa Mohamed
mwenye chupa ya maji akifunga bao hilo Moja kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Kipa wa
Bandari kuutema.
|
Ikisafiri hadi Nyakanazi,wilayani Biharamulo mkoani Kagera,Timu ya Ngara
Stars imefanikiwa kujiongezea point 3 muhimu katika harakati zake za kuwania
kombe la Mazagazaga 2014 baada ya kuifunga timu ya Bandari kutoka Biharamulo
bao 1-0.
Goli hilo la Ngara Stars lilifungwa na Mchezaji wake Wise Khalifa Mohamed
baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Kipa wa
Bandari kuutema.
Kwa ushindi huo sasa Ngara Stars imefikisha point 4 katika kundi lao la C
la Mazagazaga CUP 2014 zikiwemo pia timu za Polisi Kibondo,Cobra ya
Masumbwe,Nyakanyasi ya Bukoba na Bandari ya Biharamulo.
No comments:
Post a Comment