Wanafunzi wa
vyuo vikuu wanakusudia kufanya mgomo wa nchi nzima, kulishinikiza Jeshi la
Polisi kueleza alipo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi ya Taasisi za Elimu ya
Juu Tanzania, (Tahliso) Musa Mdede.
Mdede ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Bugando (Cuhas), mkoani Mwanza, alitoweka Jumatano iliyopita muda mfupi kabla ya kurejesha fomu ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa serikali hiyo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Baadhi ya viongozi wa wanafunzi walitangaza nia ya kufanya mgomo huo jana jijini Dar es Salaam na kulipa jeshi hilo siku moja kueleza alipo Mdede.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Spika wa Bunge wa Wanafunzii wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Yuda Gurty, alisema zimepita siku nne tangu mwenyekiti huyo atoweke kwenye mazingira ya kutatanisha na kuhoji wapi alikopelekwa.
“Tunaliagiza Jeshi la Polisi limtafute ndani ya saa zilizobaki leo kama leo hatutapata taarifa alipo tutagoma nchi nzima hadi mwenzetu atakapopatikana, tunataka walimu wafahamu hilo,” alisema.
Aliwaambia wanahabari kuwa siku ya tukio Mdede alikuwa chuoni na mara alipigiwa simu na watu wasiofahamika ambao inasemekana walikuja pale chuoni wakitumia gari lenye rangi nyeusi na kuanzia hapo alitoweka.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa taasisi hiyo, Himida Elihuruma, alisema wameshangazwa na polisi kutokana na kitendo cha kutotoa taarifa sahihi za tukio hilo.
“Tuna wasiwasi kutekwa kwa mwenzetu kunahusiana na mazingira ya kisiasa kwa sababu, Mdebe ni mtu mwenye msimamo wa kuzuia Tahliso kuwa chombo cha kutumiwa na wanasiasa,” alisema na kuongeza:
“Awali Tahliso ilikuwa ikitumiwa na wanasiasa, lakini mwenyekiti huyu alihakikisha hilo linaondoka, ndiyo maana leo tunasema msimamo wake huo unatufanya tuhusishe kutoweka kwake na siasa,” aliongeza.
Alikumbushia tukio la kutekwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka pamoja na lile la Mhariri wa gazeti lililofungiwa la Mwanahalisi, Saed Kubenea na sasa imetekwa Mdede kutokana na msimamo wake.
“… wanataka kuwaua hadi wanafunzi hatukubali tunatoa masaa tuambiwe mwenzetu alipo na iwapo yupo hai au ameshauawa,” alisema.
Mwakilishi wa Rais wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, (IFM), Musa Ndile, alisema tukio la kutekwa kwa mwenyekiti wa Tahliso limewashtua ndiyo maana wanataka kujua alipo hivi sasa.
Alisema mara nyingi wanafunzi wenye mtazamo tofauti wamekuwa wakifanyiwa matendo mabaya.
“Vyuo vikuu hatupo tayari na hatutaishia hapa, leo tutatoa kauli nyingine ambayo itahakikisha mwenzetu anapatikana na anapata haki yake ya kugombea, tumechoka kuonewa,” alisema na kuongeza:
“Matukio kama haya hata mimi yamewahi kunipata mwaka jana wakati nagombea urais ….tukio la mwenzetu sio la kwanza, tunalitaka jeshi litueleze alipo,” aliisitiza.

Chanzo:-Nipashe
Jumapili.
No comments:
Post a Comment