Imeelezwa
kuwa, tukio hilo lenye sura ya majonzi, lililovuta hisia za watu wengi
lilitokea Jumatano ya wiki hii (May 14,2014), huko King’azi, Kwembe – Mbezi, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam.
KISA CHA
YOTE
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa, chanzo cha unyama huo ni wivu wa kimapenzi ulioingilia ndoa hiyo, ambapo Gasto alimtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayeishi Temeke aliyejulikana kwa jina la Mgogo.
Chanzo chetu
cha kuaminika, kwa sharti la kutotajwa gazetini kilisema: “Mwelu na Gasto
wametoka mbali, wameishi kwa muda mrefu na wamebarikiwa watoto wawili, sema
siku za hivi karibuni, Gasto alianza kumtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa.
Bwana Gasto Edward na mkewe ambaye anadaiwa
kumkata nyeti zake.
|
“Tena siyo
tuhuma, anasema alikuwa akimwambia wazi kuwa ana mwanaume wake Mgogo ambaye
yupo Temeke. Jamaa alikuwa analalamika kuwa mkewe alifikia hatua ya kumwambia
amuache ili aende kwa mwanaume huyo anayejua kutunza.”
Akaongeza:
“Unajua katika hali ya kawaida, kama ni kweli mke alikuwa akimwambia mumewe
maneno ya hovyo kama hayo, yanaumiza. Ndiyo maana jamaa akaona kwa sababu
chanzo cha yote ni penzi, akamkata nyeti zake.”
MJUMBE
ANAFAFANUA
Mjumbe wa Mtaa wa King’azi, Amani Abdallah alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Gasto, mwezi mmoja uliopita na kufanikiwa kusuluhisha.
.......Ujumbe alioandika bwana Gasto kabla ya kutokomea............
|
“Ni kweli
walikuwa na tofauti na hili suala lilinifikia hata mimi. Gasto alikuja
kulalamika kuwa mkewe siyo mtulivu na anamwonyesha dharau.
Lakini tulisuluhisha
yakaisha. Jana (Jumatano) ambapo tukio lilitokea, yule mkewe alikuja kulalamika
kuwa mumewe amebadilika.
“Alisema
amemuona akinoa kisu asubuhi, usiku ugomvi ukatokea akaamua kuja kulala kwangu,
lakini baadaye akaniaga anakwenda kulala kwa jirani yao mama Mbonde, huko ndipo
mumewe alipokwenda kumchukua na kumfanyia unyama huo.”
WOSIA MZITO
Baada ya tukio hilo, Gasto alitoroka lakini aliandika wosia uliomtaja mrithi wa mali zake kuwa ni watoto wake Edward na Editha ambapo alimchagua kabisa msimamizi wao kuwa ni mdogo wake aitwaye Kiriani.
...........Jalada alilofunguliwa Gasto............................
|
Katika barua
hiyo, Gasto alisema anakwenda kujiua kwa sababu amechoshwa na dharau za mkewe,
ndiyo maana akaamua kuondoa sehemu zinazompa kiburi.
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa na Risasi
Jumamosi ili kuelezea tukio hilo, alikiri kupokea taarifa, akasema bado
wanafuatilia.
Habari Na:-Global Publishers.
No comments:
Post a Comment