UHALIFU:-Tazama Video ya Bibi aliyenaswa na Dawa za Kulevya nchini Tanzania alivyolia Mahakamani...'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 27, 2014

UHALIFU:-Tazama Video ya Bibi aliyenaswa na Dawa za Kulevya nchini Tanzania alivyolia Mahakamani...''





Bibi Olabisi Ibidun Cole akiangua kilio mahakamani.
Bibi wa
Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani....



Bibi wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), May 26, 2014, ameangua kilio katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa
kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37.

Hakimu aliyepelekewa kesi hiyo, Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka leo (May 27,2014) ili bibi huyo ambaye hajui Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.

Cole alisema lugha anayoweza kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini Nigeria.

Katika hali iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio akiomba
Mungu amsaidie.

(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad