![]() |
…’’..Mshtakiwa
alifanya kosa hilo May 22 ,2014, ambapo alitaka kujiua kwa kujinyonga kabla ya
kuokolewa na mtu aliyemuona akifanya jaribio hilo….’’Picha Na Maktaba Yetu.
|
Mahakama ya
wilaya ya Ngara Mkoani Kagera imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela mkazi wa
kijiji cha Mubinyange wilayani Ngara, baada ya mshitakiwa huyo kukiri kosa la
kutaka kujiua kwa kujinyonga.
Hakimu wa Makahama
ya wilaya ya Ngara Bw. Andrew Kabuka amesema mahakama hiyo imemtia hatiani Mshtakiwa
Cyprian Msigwa mwenye umri wa miaka 32 baada ya kukiri kosa la kutaka kujiua
mwenyewe.
Hakimu
Kabuka amesema Mahakama hiyo imeridhika na maelezo aliyoyatoa mshitakiwa kuwa
alitaka kujiua kutokana na kuudhiwa na mtu na kwamba ni kosa la jinai mtu
kujitoa uhai, na hivyo Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka
miwili jela.
Awali, Mwendesha
Mashitaka wa polisi Bw George Gorotto ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa alifanya
kosa hilo May 22 mwaka huu, ambapo alitaka kujiua kwa kujinyonga kabla ya
kuokolewa na mtu aliyemuona akifanya jaribio hilo.
Habari
Na:-Radio Kwizera FM.
No comments:
Post a Comment