![]() |
Kiongozi wa
Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis anakamilisha ziara yake ya siku tatu
mashariki ya kati hii pamoja na mambo mengine amewaomba waislamu kuwa na
upendo.
|
![]() |
Aliweka shada la maua katika ukumbi
huo wa ukumbusho na kusikiza hadithi za manusura wa janga hilo baya la
kihistoria kuwai kuwakumba wayahudi.
|
Kiongozi wa
Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amezungumzia janga la mateso dhidi ya
wayahudi wakati wa utawala wa Nazi- maarufu kama Holocaust, wakati wa ziara
yake katika makavazi ya Yad Vashem Holocaust mjini Jerusalem.
Aliweka
shada la maua katika ukumbi huo wa ukumbusho na kusikiza hadithi za manusura wa
janga hilo baya la kihistoria kuwai kuwakumba wayahudi.
Awali Papa
alizuru eneo la kumbukumbu la wayahudi waliouwawa kutokana na mashambulio ya
kigaidi pamoja na kuomba katika maeneo takatifu kwa waisraeli magharibi mwa
ukuta huko Jerusalem.
Papa
anakamilisha ziara yake ya siku tatu mashariki ya kati hii (May 26,2014) kwa kuzuru
msikiti wa zamani wa al-Aqsa na kuwaomba waislamu kuwa na upendo.
Viongozi hao
wawili Shimon Peres wa Israel na Mahmoud Abbas wa Palestina wameelezea matumani
ya kumtemblea Papa.
Akiongea na
mufti wa Jerusale, Ppa alitoa wito kwa wakristo, wayahudi na waisilamu
kupendana.
No comments:
Post a Comment