![]() |
Mtoto akiwa
kwenye tumbo la Mama yake ambapo Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito
wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri
shuleni.
|
Utafiti
uliofanywa na shirika la African Council for Gifted and Talented unaonyesha
kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawamakiniki
darasani.
Mkuu wa
shirika hilo Profesa Humprey Obora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa
utafiti huo umefanywa kwa watoto wanaopelekwa katika taasisi hiyo ambayo
hujihusisha kutambua na kukuza vipawa vya watoto wakiwa bado wachanga.
![]() |
Udongo
unaoliwa na wanawake
katika
baadhi ya nchi Afrika
|
Zaidi ya
wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao
yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.
Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.
Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.
Wasimamizi wa mradi huo waliwahusisha wazazi kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ambako kuna vituo vya shirika la African Council for Gifted and Talented.
Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo.
No comments:
Post a Comment