Bendi ya
muziki wa dansi nchini Tanzania Mashujaa, inatarajia kufanya ziara katika mikoa yote
nchini nzima kwa ajili ya kutoa shukrani kwa mashabiki wao waliowapigia kura
kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Awards.
Akizungumza Dar es Salaam jana (May 22,2014) , Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi hiyo Maximillian Luhanga, alisema kuwa wamepata mafanikio makubwa kwa miaka miwili baada ya kupata tuzo nane.
Alisema kuwa mwaka jana (2013) walipata tuzo tano na mwaka huu ( 2014) wamefanikiwa kupata tuzo tatu kutokana na kura za mashabiki wao.
“Tunatarajia kufanya ziara katika mikoa yote ya Tanzania baada ya kupata tuzo tatu mwaka huu na hivyo hiyo ziara itakuwa kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wetu,” alisema.
Alisema kuwa wamesharekodi nyimbo mbili mpya ambazo watazitumia mikoani ikiwa ni kama zawadi kwa mashabiki wao, ambapo nyimbo hizo ni Usidharau Sifuri na Kiu ya Haki.
Alisema kuwa ili waendelee kuwa karibu na mashabiki wao kila mwezi watakuwa wanatengeneza matukio mbalimbali ya bendi katika mitandao ya Kijamii.
KUPATA
HABARI / NYIMBO KUHUSU MASHUJAA BAND INGIA HAPA ZAIDI>>>>>https://www.facebook.com/mashujaaband?fref=ts
No comments:
Post a Comment