Meneja Biashara ya Petroli wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) nchini Tanzania, Julius Gashaza enzi za uhai
wake.
|
Hii ni Hoteli aliyodaiwa kulala Meneja huyo wa Ewura. |
.......Chumba alichodaiwa kulala Meneja wa Ewura....... |
![]() |
..................Hiki ni choo alichokutwa meneja huyo............ |
![]() |
....Meneja Gashanza (mwenye kofia) akiwa kazini enzi za uhai wake........ |
Aliyekuwa Meneja wa Biashara
ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza anazikwa
leo (May 22, 2014) katika Kijiji cha Murukulazo, wilayani Ngara mkoani Kagera
huku familia yake ikisema haina cha kusema kuhusu kifo hicho, bali inamwachia
Mungu.
Akizungumza kijijini hapo, mdogo wa marehemu, Alex Gashaza
alisema familia imepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kushangazwa na taarifa
kwamba ulitokana na kujinyonga kama inavyodaiwa.
Alisema baada ya kupokea simu
kutoka Dar es Salaam kuhusu mazingira ya kifo hicho, wameshindwa kujua sababu
za kifo kwa kuwa hakuna mtu aliyezungumza naye.
Alisema kaka yake hakuwa na
tatizo lolote na wanafamilia, ndugu wala jamaa zake wa karibu, hivyo familia
haiwezi kuelezea jambo ambalo halina ushahidi, badala yake inaacha tukio hilo
mikononi mwa Mungu.
Mwili wa Gashaza baada ya kuwasili
Murukulazo jana (May 21,2014) jioni na leo saa 4:00 asubuhi utapelekwa katika
Kanisa la Anglikana katika kijiji hicho kwa ajili ya sala na saa 6:00 mchana
utaagwa kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake.
Kiongozi wa Kanisa la
Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza mkoani Mwanza, Mchungaji Lazaro
Manjelenga ambaye pia ni baba mkwe wa mdogo wa marehemu, alisema wana matumaini
na Muumba kwa kile kilichotokea.
“Siri ya Mungu na mwanadamu
wake hakuna wa kuijua, hivyo tusihukumu,” alisema na kuongeza kuwa mazishi
yatafanyika kwa mujibu wa taratibu za Kanisa hilo.
MASWALI MATANO KIFO CHA MENEJA EWURA.
Swali la kwanza:- Kama kweli
marehemu alinyongwa ni kwa nini mlango ulikutwa umefungwa kwa ndani? Je,
mnyongaji alitokaje baada ya kutekeleza mauaji hayo?
Swali la pili:- Kama kweli
marehemu alinyongwa, kwa nini kitandani kulikutwa na alama ya mtu kukaa tu na
kusiwepo kwa dalili za mapambano au purukushani?
Swali na tatu:- Kama kweli
alijinyonga mwenyewe ni kwa nini iwe kipindi hiki ambacho inadaiwa alipokea
vitisho kutoka kwa wabaya wake kwamba atauawa?
Swali la nne:- Uamuzi wa
kuchukua chumba kwenye hoteli hiyo ulitoka kwa nani? Marehemu mwenyewe au? Kama
alishauriwa, aliyemshauri ana cha kujibu?
Swali la tano:- Kama kulikuwa
na matatizo ya kikazi kama ilivyodaiwa, basi Mkurugenzi Mstaafu wa Ewura,
Haruna Masebu atakuwa anayajua hivyo angeweza kusaidia kuyasema.
Swali lingine ambalo
lingeweza kuongeza idadi ni juu ya uwezekano wa kuingizwa kwa funguo nje wakati
ya ndani ilizungushwa lakini imebainika kwamba baada ya funguo kufungwa na
mlango kuwa ‘lokdi’, funguo hiyo huwa ‘luzi’ tena hivyo mwenye funguo nje
anaweza kuisukuma na kuingiza nyingine.
Aidha tayari Jeshi la Polisi
limeunda jopo la Upelelezi kuchunguza kifo hicho cha Gashaza kinachodaiwa
kutokea katika mazingira ya kutatanisha na kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar
es Salaam,Suleiman Kova alisema kuwa Jopo hilo litaongozwa na Mkuu wa Upelelezi
kanda hiyo Jaffar Mohamed akishirikiana na wataalamu wa Maabara kuu ya Polisi,Daktari
Bingwa wa Polisi na Serikalini.
Kamanda Kova amesema jeshi hilo
linafanya uchunguzi ili kuoandoa utata ulioanza kujitokeza kuhusiana na kifo chake
baada ya taarifa kuzaga kwamba kilitokana na kutoelewana na Viongozi wenzake katika
Masula ya kikazi.
Alisema uchunguzi huo ukikamilika
,Jalada litapelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali ili hatua za kisheria zichukuliwe.
No comments:
Post a Comment