Waziri wa Ujenzi, Dk. John
Pombe Magufuli akiwasilisha hotuba yake ya Bajeti ya mwaka 2014/2015 Bungeni
Mjini Dodoma.
|
Waziri Willium Lukuvi na
Naibu Waziri Januari Makamba wakijadiliana jambo Bungeni mjini Dodoma.
|
Wizara ya Ujenzi ya Tanzania imepanga
kujenga barabara 41 na madaraja 13 nchini kwa kiwango cha Lami zenye urefu wa
kilomita 3,074, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa barabara ya Dar es
Salaam-Chalinze yenye urefu wa kilomita 100 kwa mwaka 2014/15.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John
Magufuli, akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/15,
alisema ujenzi wa barabara na madaraka hayo utagharamiwa na serikali na
wahisani.
Alisema barabara ya Dar es
Salaam-Chalinze- Morogoro (km 200) kwa kiwango cha 'Expressway' utagharimu Sh.
milioni 750 na kwamba maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo yanaendelea na
utatekelezwa baina ya serikali na sekta binafsi.
Dk. Magufuli alisema awamu ya
kwanza itakuwa kilomita 100 kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze na kiasi cha
Shilingi milioni 100 zimetegwa.
Alisema barabara nyingine ni
Wazo hill-Bagamoyo itakayogharimu shilingi milioni 10,885.24 ikiwa ni pamoja na
kujenga kwa kiwango cha lami sehemu ya Bagamoyo-Makofia-Msata kilomita 64 na
ujenzi wa daraja la Ruvu Chini.
Barabara nyingine ni
Usagara-Geita-Kyamyorwa kilomita 422, kigoma -Kigahwe-Upinzani-Kaliua -Tabora,
Marangu -Tarakea-Kimwanga-Bomong’ombe- Sanya Juu yenye urefu wa kilomita 173, Arusha
-Moshi-Holili kilomita 140, lengo ni kuchochea ukuaji wa Utalii katika Mlima Kilimanjaro.
Nyingine ni Same -Himo
–Marangu- Rombo -Lushoto kilomita 132, Kia-Mererani kilomita 26, Kwa Sadala Machame-Masama-Machame kilomita 15.5
na Kiboroloni Kiharara-Tsudini-Kidia kilomita 10.80 zote zikigharimu Sh.
milioni 13.133.63.
Barabara ya
Nangurukuru-Mbwemkulu kilomita 95, Dodoma - Manyoni Kilomita 127,
Mbwemkuru-Mingoyo kilomita 95, Dumila - Kilosa kilomita 78, Sumbawanga -Matai-
Kasanga kilomita 112.
Nyingine ni
Kayka-Bugene-Kasulu kilomita 178, Isaka-Lusahunga kilomita 242 na
Lusahunga-Rusumo na Nyakasanza -Kobera kilomita 150, Manyoni-Itigi -Tabora na
Korogwe -Handeni.
Madaraja yatakayojegwa ni ya
Kirumi, Nangoo, Sibiti, Maligisu, Kilombero, Kavuu, Mbutu, Rehekei, Ruhuhu,
Mombo, Simiyu, Wami na Lukuledi II. Hata hivyo, urefu wake haukutajwa.
Alisema baadhi ya barabara
ilishaanza ujenzi na nyingine ndiyo zitaanza huku madaraja yakiwa katika hatua
mbalimbali ya ujenzi na mengine yakihitaji upanuzi.
Barabara za mikoa
zitakazokarabatiwa ni za kilomita 685 za
changarawe na za lami kilomita 78.
Aidha Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania jana (May 21,2014) Limepitisha Bajeti ya Wizara hiyo yenye
Jumla ya shilingi Trilioni 1 na bilioni
219,milioni 717 na laki 592.
No comments:
Post a Comment