REST IN PEACE:-Marehemu Julius Gashaza-Leo May 22, 2014- Mazishi yake yakifanyika Murukulazo,Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 22, 2014

REST IN PEACE:-Marehemu Julius Gashaza-Leo May 22, 2014- Mazishi yake yakifanyika Murukulazo,Ngara mkoani Kagera.


Jeneza la mwili wa Marehemu Julius Gashaza aliyefariki usiku wa kuamkia Jumapili (May 18,2014) akiwa hotelini jijini Dar es Salaam, huku kifo chake kikionekana kutokea katika mazingira ya kutatanisha ambapo Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Costantine Kanyasu, amewaongoza viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa na Mamia ya Wananchi katika Mazishi yake leo (May 22, 2014) Kijijini kwao Murukulazo wilayani Ngara.

Ibada ya mazishi hayo iliongozwa na Vika General wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kagera ,Mchungaji Philipo Mvunyi  pamoja na mambo mengine amesema wanafamilia, ndugu na jamaa wachukulie msiba huo kama mapenzi ya mungu kwa kuwa kila mwanadamu ameandikiwa mazingira ya kuondoka hapa duniani.

Salamu mbalimbali za rambirambi zilitolewa kwa Familia ya Marehemu ambapo  Mkurugenzi wa Mafuta wa EWURA Bw Godwin Samwel amesema kuwa Marehemu ameacha pengo kubwa katika Mamlaka hiyo, kwani alitegemewa kwa kiasi kikubwa katika uadilifu wake kiutumishi.

.....Mamia ya Wananchi mbalimbali waliohudhuria Mazishi ya aliyekuwa Meneja wa Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza aliyefariki May 18,2014,Maziko yake yamefanyika leo (May 22, 2014) Kijijini kwao Murukulazo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Hii ndio nyumba ya milele ya Marehemu Julius Gashaza:- BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE…’’



Baada ya Ibada ya Mazishi ya Meneja wa EWURA-Julius Gashaza kukamilika  ,sasa amepelekwa kwenye Nyumba yake ya Milele.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad