Ajali hiyo ilitokea Aprili 28,2014,majira ya saa 2.45 usiku katika barabara kuu ya
Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi
mkoani Singida.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP,Geofrey Kamwela amesema
kwa sasa wanaendelea na taratibu za kisheria na watakapomaliza pamoja na
upelelezi,dereva Paul aftafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia
tiketi ya CHADEMA,Tundu Lissu,ameahidi kutoa msaada wa kisheria kwa ndugu
waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya basi la Summry.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na
Diwani wa kata ya Mungaa (CHADEMA) Mtheo Alex wakati akizungumza kwenye hafla
ya sala maalum ya kuombea watu 14 wakazi wa kijiji cha Utaho waliogongwa na
basi la Summry.
Amesema mbunge huyo anatafuta
nafasi ili afike kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa na vile vile
atashughulikia taratibu zote za fidia zitakazotokana na basi hilo T.799
BET mali ya kampuni ya Summry.
“Taratibu za bima huwa si za
kumalizika kwa muda mfupi,kawaida huwa za muda mrefu,kwa hiyo ndugu zanguni,
kwa hili tuwe wavumilivu na tuendelee kuamini kwamba mwanasheria wetu
Tundu,atalimudu”,amesema.
Wakati huo huo, Diwani wa kata ya
Kituntu (CCM),Naftali Gwae alikanusha uvumi kuwa rais Jakaya Kikwete alituma
rambai rambi zikiambatana na fedha.
“Rais wetu alituma salamau za rambi rambi na wala
sio fedha.Kwa hiyo ndugu zangu niwasihi tu kwamba wakati huu mgumu unaoambatana
na majonzi,mengi yatasemwa mengi lakini tuwe makini na kuyafanyia
uchunguzi kwanza”,amesema.
Aidha,uvumi ulioenea kwamba Diwani wa CCM na Mtendaji wamechukua
kutoka ofisi ya kijiji nyaraka za benki zinazodaiwa kuonyesha kuwa kijiji hicho
kina akaunti yenye zaidi ya shilingi milioni mia moja,si za kweli ni uongo
mtupu.
Kwa mujibu wa Diwani Gwae baada ya sala hiyo,waathirika wa ajali
hiyo kila moja amepewa shilingi 212,500 ikiwa ni rambarambi kwa kupoteza ndugu.
Fedha hizo ni kutoka fedha za ubani za shilingi Milioni 5 zilizotolewa na
mmiliki wa kampuni ya Summry,shilingi laki moja mkuu wa mkoa wa Singida na
shilingi 150,000 zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha Minyinga.
No comments:
Post a Comment