PICHA / HABARI:-Tazama matukio mbalimbali ya Ufunguzi wa Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera leo May 24,2014-Chuo cha Ualimu Katoke. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 24, 2014

PICHA / HABARI:-Tazama matukio mbalimbali ya Ufunguzi wa Mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera leo May 24,2014-Chuo cha Ualimu Katoke.


Kikosi cha Wanamichezo 71 cha Shele za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Ngara waliochaguliwa kuunda timu ya UMISETA 2014 Ngazi ya Mkoa wa kagera wakitoa salamu kwa Mkuu wa Mkoa huo ,Kanali mstaafu Fabiani Massawe wakati wa Ufunguzi wa Mashindano hayo  ya michezo kwa umoja wa shule za sekondari Ngazi ya mkoa kwa Mkoa wa Kagera leo jumamosi May 24, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba.




.............Wanaonekana nao bado wamo.....ni Viongozi wa Kikosi cha Wanamichezo 71 cha Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Ngara waliochaguliwa kuunda timu ya UMISETA 2014 Ngazi ya Mkoa wa kagera wakiwa katika maandamano ya pamoja wakati wa Ufunguzi wa UMISETA Ngazi ya mkoa  May 24, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba.........



Waamuzi wa Michezo ya soka wanaume na wanawake ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa kagera nao walipita kutoa salamu yako kwa  Mkuu wa Mkoa huo ,Kanali mstaafu Fabiani Massawe wakati wa Ufunguzi wa Mashindano hayo  ya michezo kwa umoja wa shule za sekondari Ngazi ya mkoa kwa Mkoa wa Kagera leo jumamosi May 24, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba.


Kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali mstaafu Fabiani Massawe wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya UMISETA 2014 leo jumamosi May 24, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke wilayani Muleba..anaefata ni Makamu Mwenyekiti UMISETA mkoa na Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Ngara,Julius Nestory na viongozi wengineo.


Viongozi hao pamoja na Wanamichezo 577,wanawake wakiwa 268 kwa pamoja na watazamaji waliojitokeza waliimba nyimbo za Kizalendo ukiwemo wa AMANI NA MAENDELEO mkoani Kagera.


....................wakiimba....Amani na Maendeleoo.........Kagera...............



Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera –Fabiani Masawe akipiga mpira kumfunga golikipa wa timu ya soka ya wanawake ya Muleba kama ishara ya ufunguzi wa mashindano ya UMISETA 2014 Ngazi ya mkoa wa Kagera leo Jumamosi May 24,2014 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Katoke.


Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera –Fabiani Masawe akisalimiana na wachezaji wa Timu ya soka ya Halmashauri ya wilaya ya Ngara kabla ya mchezo wao dhidi ya Kyerwa ,nyuma yake Julius Nestory-makamu mwenyekiti UMISETA mkoa na Kepha Elias Mwenyekiti/Afisa Michezo mkoani Kagera.

Mashindano ya michezo kwa umoja wa shule za sekondari Ngazi ya mkoa kwa Mkoa wa Kagera yamezinduliwa rasimi leo jumamosi May 24, 2014 na mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanal mstaafu Fabiani Masawe.

Akifungua mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu katoke wilayani Muleba,Kanali Massawe amesema kuwa licha ya azma ya Serikali kutekeleza sera ya michezo nchi,wakati umefika sasa kwa Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoani humo nao kuhudhuria Mashindano hayo ya UMISETA  ili kuwa chachu ya kuendeleza michezo katika wilaya zao.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera –Fabiani Masawe amewataka washriki wa mashindano ya UMISETA kwa mwaka huu kuonyesha nidhamu na bidii wakati wa mashindano ili vipaji vyao vionekane na kuendelezwa.

Awali akimkaribisha Mgeni rasimi katika ufunguzi huo,Makamu mwenyekiti wa UMISETA mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa UMISETA wilaya ya Ngara-Julius Nestori amesema kuwa mashindano hayo kwa mwaka huu yanashirikisha yanashirikisha wanamichezo 577 kutoka wanafunzi waliochaguliwa katika shule za sekondari za wilaya 8 za mkoa wa Kagera na yana lengo la kupata timu ya UMISETA mkoa wa Kagera.

Wilaya hizo ni Manispaa,Bukoba Vijijini,Karagwe,Kyerwa,Misenyi,Ngara,Biharamulo na Muleba.

Mara baada ya ufunguzi-Timu ya soka ya UMISETA ya Halmashauri ya wilaya ya Ngara iliingia dimbani kupambana na wenzao wa Kyerwa katika uwanja wa soka wa chuo cha Katoke na kufanikiwa kuwafunga bao 2-1 magoli ya ushindi ya Ngara yakifungwa na Antoni Oscar na Maziku Katika mchezo wa soka la wanawake,Timu ya soka ya UMISETA ya Halmashauri ya Bukoba  iliwanyanyasa vilivyo wenzao wa Biharamulo kwa kuwatandika magoli  6-0.

Mwenyekiti wa UMISETA au Afisa Michezo mkoa wa Kagera-Khepa Eliasi amesema kuwa UMISETA ngazi ya kikanda ili kupata timu ya ZIWA MAGHARIBI- sasa itafanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu Katobe kuanzia May 31,2014 badala ya Geita kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad