MWENGE WA UHURU 2014:-Wawasha Mkoani Kagera na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr.Bilal na Kauli mbiu:- "JITOKEZE KUPIGA KURA YA MAONI TUPATE KATIBA MPYA". - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 03, 2014

MWENGE WA UHURU 2014:-Wawasha Mkoani Kagera na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr.Bilal na Kauli mbiu:- "JITOKEZE KUPIGA KURA YA MAONI TUPATE KATIBA MPYA".


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera, Mei 2, 2014. . Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera, Mei 2, 2014.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera , Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR


Mwenge huo wa Uhuru 2014,unaoongozwa na Rachael Stephen Sanda kutoka mkoa wa Tabora, ambapo ukiwa katika Manispaa ya Bukoba umezindua miradi 10  ya Kimaendeleo na kulala kata ya Kashai ili kuelekea wilaya za Muleba, Bukoba Vijijini, Misenyi ,wilaya za Kyerwa na Karagwe na kuhitimisha mbio zake mkoani Kagera na wilaya ya  Ngara tarehe 14,May 2014, utakapokabidhiwa kwa mkoa wa Kigoma.


Vijana wenye dhamana ya kukimbiza mwenge wa Uhuru 2014, wakianza rasmi mbio hizo baada ya kuwashwa na kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera , Mei 2, 2014. Picha na OMR


Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akishiriki kuimba wimbo wa Taifa.


Vijana wa Haraiki wakionyesha umahiri wao kwa kutoa burudani wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera jana Mei 02, 2014. ...Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 ,2014,mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR.



Wasanii wa bendi ya Kakao ya mjini Bukoba, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za kuuwasha Mwenge wa Uhuru .


Msanii wa muziki wa Kizazi kipya kutoka mjini Zanzibar, It, akiimba wimbo maalumu wa kuhamasisha mbio za mwenge.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera jana Mei 02, 2014. ...Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 ,2014,mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR



Baadhi ya wageni waalikwa, Wakuu wa Wilaya za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, waliohudhuria sherehe hizo za uzinduzi. Picha na OMR.

Picha juu na chini ni Vijana wa Haraiki wakionyesha umahiri wao kwa kutoa burudani wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera jana Mei 02, 2014. ...Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 ,2014,mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR.


Baadhi ya wageni waalikwa, Wakuu wa Wilaya za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, waliohudhuria sherehe hizo za uzinduzi. Picha na OMR.


Kauli mbiu ya mwaka huu 2014:- "JITOKEZE KUPIGA KURA YA MAONI TUPATE KATIBA MPYA".

Mwenge huo wa Uhuru 2014,unaoongozwa na Rachael Stephen Sanda kutoka mkoa wa Tabora, ambapo ukiwa katika Manispaa ya Bukoba umezindua miradi 10  ya Kimaendeleo na kulala kata ya Kashai ili kuelekea wilaya za Muleba, Bukoba Vijijini, Misenyi ,wilaya za Kyerwa na Karagwe na kuhitimisha mbio zake mkoani Kagera na wilaya ya  Ngara tarehe 14,May 2014, utakapokabidhiwa kwa mkoa wa Kigoma.

Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilal ametumia ujumbe wa mbio hizo mwaka huu 2014, kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi, katika kuipitisha kwa kuipigia kura rasimu ya katiba Mpya mara Bunge Maalum la Katiba litakapokamilisha kazi ya kuijadili.

Aidha Dk.Bilal ametoa wito kwa Wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyoshughulikia udhibiti wa dawa za kulevya ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Amesema kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na vyombo hivyo bado tatizo la dawa za kulevya ni kubwa na kuwataka wananchi kuwataja waagizaji na wasambazaji wa dawa hizo ili wachukuliwe hatua.

Kauli mbiu ya mwaka huu 2014:- "JITOKEZE KUPIGA KURA YA MAONI TUPATE KATIBA MPYA". 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad