|
Wafuasi na
wapenzi wa vyama vya upinzani wakifuatilia mkutano wa UKAWA uliofanyika viwanja
vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba. Na Umoja huo wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA), umesema utaendelea na kampeni yake ya kutembea nchi nzima
kuwafahamisha wananchi juu ya malengo ya umoja huo pamoja na mustakbali wa
katiba mpya ya Tanzania.
|
|
Akihutubia
mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa viongozi wa Ukawa katika viwanja vya
Gombani ya kale Chake Chake Pemba, kiongozi wa Umoja huo,Bw.Freeman Mbowe amesema
umoja huo umekusudia kuwaungunisha watanzania, ili wapate katiba mpya
inayotokana na maoni na kuzingatia maslahi yao.
Amefahamisha
kuwa umoja huo una dhamira ya kweli, na kwamba kuanzia sasa hawatokuwa tayari
kugawanywa kwa misingi udini, ukabila au maeneo.
Mbowe ambaye
ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kwa
kipindi kirefu vyama vya upinzani vimekuwa vikibaguliwa kwa misingi hiyo, na
kuahidi kuwa vitendo hivyo sasa vimefikia mwisho.
“Sisi
CADEMA tumezushiwa propaganda kuwa ni chama cha Kikristo, na wenzetu wa CUF
wakaambiwa kuwa ni chama cha Kiislamu. Sasa tumegundua kuwa lengo lao ni
kutugawa na sasa hatugawiki tena”, alisisitiza Mbowe.
Kufuatia
kusonga mbele kwa UKAWA, Bw.Mbowe ambaye ni Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani
bungeni, amesema atavunja na kuunda upya baraza la mawaziri kivuli bungeni ndani
ya saa 24, ili kuwashirikisha viongozi wengine wanaounda umoja huo.
|
|
Mwenyekiti
wa NCCR Mageuzi ,Bw.James Mbatia, amesema kitendo cha baadhi wa viongozi wa
serikali kwamba iwapo muundo wa serikali tatu utakubaliwa, Zanzibar itakuwa
dola ya kiislamu ni chokochoko ambazo hazina ukweli.
Amefahamisha
kuwa Waislamu na Wakristo wa Zanzibar wana uhusiano wa muda mrefu na wa
Kihistoria ambao hauwezi kutenganishwa, huku akielezea historia ya kanisa la
Minara Miwili la Zanzibar ambalo ni miongoni mwa makanisa yenye historia ndefu
katika ukanda wa Afrika Mashariki.
|
|
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, amerejea kauli zake kuhusu
matumizi mabaya ya fedha za umma ndani ya serikali, na kwamba ikiwa vitendo
hivyo vitaachiwa kuendelea, nchi itashindwa kupiga hatua za maendeleo kwa
haraka. |
|
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewashukuru viongozi wa UKAWA kwa
kuonesha umahiri ndani na nje ya bunge, na kuahidi kushirikiana nao katika
harakati za kupata katiba mpya inayotokana na mawazo ya wananchi. |
|
Baadhi ya
viongozi wa UKAWA na wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba Maalim Seif,
katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake
Pemba.
|
|
Viongozi hao
kwa pamoja wamewapongeza wananchi wa Pemba kwa kuonyesha mshikamano katika
kupigania haki na maendeleo ya kisiwa hicho, na kwamba ni mahali pazuri pa
kujifunza mshikamano. |
Pia Umoja
huo wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umetangaza dhamira yake ya kutaka vyama
vinavyounda umoja huo kumsimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi mkuu mwaka
2015.
UKAWA
unajumuisha vyama vya upinzani vya CUF, CHADEMA, DP na NCCR- Mageuzi ambavyo
viongozi wake wako pamoja katika mikutano ya hadhara inayoendelea nchini.
No comments:
Post a Comment