LA LIGA 2013/2014:- FC Barcelona yashindwa kuizuia Atletico Madrid kuwa Bingwa wa La Liga huku Kocha Gerardo Martino Akibwaga Kibarua Chini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 18, 2014

LA LIGA 2013/2014:- FC Barcelona yashindwa kuizuia Atletico Madrid kuwa Bingwa wa La Liga huku Kocha Gerardo Martino Akibwaga Kibarua Chini.


Atletico Madrid May 17, 2014- Ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Hispania - La Liga 2013/2014  baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao  1-1 na FC Barcelona kwenye uwanja wa Camp Nou…..Hilo linakuwa taji la 10 la Atletico katika Ligi ya La Liga, baada ya awali kutwaa katika misimu ya mwaka 1939 / 1940, 1940 / 1941, 1949 / 1950, 1950 / 1951, 1965 / 1966, 1969 / 1970, 1972 / 1973, 1976 / 1977 na 1995 /1996.


Kwenye Mechi hii, Atletico walimpoteza Mfungaji wao Bora, Diego Costa, ambae alilazimika kutoka baada kuumia…pia  wamemaliza La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Barcelona na Real Madrid katika Msimamo wa Ligi wakiwa na Point 87 kwa Real Madrid wameaga vyema Santiago Bernabeu baada kuichapa Espanyol Bao 3-1.


Atletico Madrid players wakifurahi baada ya mchezo kumalizika dhidi ya Barcelona lna kuchukua Ubingwa wa La Liga to a first title since 1996.


FC Barcelona ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 32 kwa Bao la Alexis Sanchez na Atletico kusawazisha Dakika ya 49 kwa Bao la Diego Godin….Aidha, hii inakuwa mara ya kwanza baada ya miaka tisa kwa timu nje ya Barcelona na Real Madrid kutwaa taji hilo, mara ya mwisho Valencia walikuwa mabingwa msimu wa 2003-2004. 


Atletico Madrid wanashinda Kombe la La Liga kwa mara ya kwanza toka mwaka  1996 baada ya kudroo goli 1-1 na FC Barcelona.

Last 11 La Liga winners.

  • 2014: Atletico Madrid
  • 2013: FC Barcelona
  • 2012: Real Madrid
  • 2011: FC Barcelona
  • 2010: FC Barcelona
  • 2009: FC Barcelona
  • 2008: Real Madrid
  • 2007: Real Madrid
  • 2006: FC Barcelona
  • 2005: FC Barcelona
  • 2004: Valencia

League Table La Liga 2013/2014.

Position Team Played Goal Difference Points
1 Atlético Madrid 38 51 90
2 Barcelona 38 67 87
3 Real Madrid 38 66 87
4 Athletic Bilbao 37 27 69
5 Sevilla 37 15 60
6 Real Sociedad 37 8 59
7 Villarreal 37 15 56
8 Celta de Vigo 37 -4 49
9 Levante 38 -8 48
10 Valencia CF 37 -3 46
11 Málaga 38 -7 45
12 Rayo Vallecano 37 -33 43
13 Espanyol 38 -10 42
14 Elche 37 -18 40
15 Almería 37 -28 39
16 Getafe 37 -20 39
17 Granada CF 37 -25 38
18 Osasuna 37 -31 36
19 Real Valladolid 37 -21 36
20 Real Betis 37 -41 25


Kocha  Gerardo Martino amesema anaondoa Barcelona baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza kazini vibaya akikosa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Atletico Madrid. 

Kocha huyo Muargentina amefikia makubaliano ya kuacha kazi baada ya Barcelona kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wapya wa msimu wa 2013/2014, Atletico Madrid.

Martino aliteuliwa kuifundisha Barcelona msimu huu wa 2013/2014 ili kuendeleza wimbi la mafanikio Barcelona lililoanzishwa na Pep Guardiola mwaka 2008. 

Lakini Barcelona imemaliza msimu bila taji lolote kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2007-08. 

Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi ya Martino, ambaye anaondoka akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.

Enrique anaachia ngazi ukocha wa Celta Vigo baada ya kukutana na Barcelona wiki iliyopita.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad