TASWIRA:Tazama Picha 12 za mkutano wa UKAWA leo April 30, 2014-Kibandamaiti Zanzibar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 30, 2014

TASWIRA:Tazama Picha 12 za mkutano wa UKAWA leo April 30, 2014-Kibandamaiti Zanzibar.

Wakazi wa kutoka kisiwa cha Tumbatu,Zanzibar wakihudhuria mkutano wa UKAWA na Mabango yao leo April 30, 2014-kiwanja cha Kibandamaiti-Zanzibar.


Muasisi,Mzee Nasoro Moyo naye alifika kwenye mkutano huo wa UKAWA.

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu mkuu wa CUF,Maalim Seif  Sharif Hamadi akikumbatiana na Katibu mkuu wa CHADEMA,Dr.Wilbroad Slaa ,kulia kwake ni Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi Bw.Musona.


Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu mkuu wa CUF,Maalim Seif  Sharif Hamadi akisalimiana na Wananchi katika mkutano wa UKAWA leo April 30, 2014 katika viwanja vya Kibandamaiti,Zanzibar.

Picha juu na Chini ni Wananchi wakifatilia na kushangilia kile kilichokuwa kinaendelea  katika mkutano wa UKAWA leo April 30, 2014 katika viwanja vya Kibandamaiti,Zanzibar.


Wenyeviti wa vyama vitano vya upinzani nchini Tanzania vilivyoungana na kuunda UKAWA,Bw.James Mbatia wa NCCR –Mageuzi,kushoto-Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF katikati na kulia kwake ni Mwenyekiti wa CHADEMA Bw.Freeman Mbowe wakiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa UKAWA leo April 30, 2014,kwenye viwanja vya Kibandamaiti-Zanzibar.


Picha chini na juu ni Muonekano wa Mabango yenye ujumbe yaliyobebwa na Wananchi kuonyesha kuunga mapendekezo ya Wananchi ya kutaka Serikali 3 kwenye rasimu ya pili ya katiba ya Tanzania ambayo sasa imewasilishwa katika Bunge maalumu la Katiba kuijadili na litarejea Agost 05,2014 kuendelea na mjadala wa rasimu hiyo.


Mwananchi huyu alikuwepo katika mkutano wa UKAWA leo April 30, 2014,Mjini Zanzibar na akaonyesha picha aliyoiweka mgongoni mwake ya Rais mstaafu wa Zanzibar naye anataka Serikali 3.


Mkutano wa umoja wa katiba ya Wananchi-UKAWA- uliozuiliwa na jeshi la polisi mara mbili umefanyika leo(April 30,2014) katika uwanja wa Kibandamaiti mjini Zanzibar huku viongozi wakuu wa vyama  vitano vya upinzani wakihudhuria  na kuhutubia.

Mkutano huo ulihudhuriwa na mamia ya wanachama,wapenzi na wananchi kwa mara ya kwanza kushuhudia mkutano wa kisiasa ukihutubiwa na viongozi wakuu na makatibu wa vyama vitano vikuu vya upinzani nchini Tanzania, ambapo katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF,Maalim Seif Sharrif Hamadi  ambaye alikuwa Mwenyeji wa mkutano huo alitamka kuinga mkono UKAWA, huku wa Kwanza kuanza kuanika nguvu zake za kudai serikali tatu alikuwa Mwenyekiti wa  Chama cha NLD,Bw.Emamanuel Makaidi ambaye alisema Tanganyika lazima ipatikane.

Na ndipo wakafuatiwa na wenyeviti wa NCCR-Mageuzi ,Bw.James Mbatia ambaye alifafanua kuhusu rasimu hiyo na utaratibu wake  huku Mwenyekiti wa CHADEMA,Bw.Freeman Mbowe kwa upande wake  ametangaza rasmi  kuwa umoja mpya wa vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 utasimamisha mgombea wao pamoja na kulitangaza upya baraza la Mawaziri kivuli Bungeni na mwisho alikuwa Mwenyekiti wa CUF,Professa Ibrahim Lipumba ambaye aliifafanua rasimu ya pili ya katiba kwa mapendekezo ya wananchi  na kuwapinga wanaopigia debe seriklai mbili.

Aidha huo ni mkutano mkubwa na wa kwanza kufanyika huko Zanzibar kuhusu rasimu ya Katiba ambapo umoja huo wa UKAWA sasa unaelekea kiiswani pemba kwa kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad