Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara ,msimu wa 2013/2014, inafikia tamati yake Jumamosi Aprili 19,2014, na Mechi zote ni za
kukamilisha Ratiba tu kasoro ile itakayochezwa huko Uwanja wa Jamhuri, Morogoro
kati ya Ashanti United na Tanzania Prisons ambayo itaamua nani wanaungana na
JKT Oljoro na Rhino Rangers kucheza Daraja la Kwanza, FDL, Msimu ujao wa 2014/2015.
Hali hii ni
kwamba tayari Bingwa ameshapatikana ambae ni Azam FC na Timu ya Pili ni Yanga SC.
Lakini pia
ipo Mechi tamu kwa Mashabiki wa Kandanda Tanzania na si nyingine bali ni ile
Dabi ya Kariakoo inayokutanisha Miamba ya Soka, Yanga SC na Simba SC, ambazo
zikikutana hamna masihara ni kazi kweli kweli na vidole machoni.
Timu hizi
zilitoka Sare ya Bao 3-3 katika Mechi yao ya Kwanza ya Ligi ambapo Yanga
SC waliongoza 3-0 hadi Mapumziko na Simba SC kusawazisha Bao zote Kipindi cha Pili.
Baada ya
hapo, Yanga SC na Simba SC zilikutana Mwezi Desemba,2013 kwenye lile pambano la Nani Mtani
Jembe na Simba SC kuibuka kidedea kwa Bao 3-1.
Pia wale
Wadau safi wa Soka watataka kujua ikiwa Mabingwa wapya, Azam FC, ambao wamefuta
mwiko wa Yanga SC na Simba SC kupokezana Ubingwa tangu Mwaka 2000 walipochukua Mtibwa
Sugar kwa mara ya mwisho, wataweza kudumisha Rekodi yao murua ya kutofungwa
Mechi hata moja ya Ligi Msimu huu watakapofunga dimba dhidi ya JKT Ruvu huko
Azam Complex, Chamazi, Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Mechi za
mwisho za Ligi
Jumamosi
Aprili 19,2014.
Rhino
Rangers v Ruvu Shooting [Ali Hassan Mwinyi, Tabora]
Mbeya City v
Mgambo JKT [Sokoine, Mbeya]
Tanzania
Prisons v Ashanti United [Jamhuri, Morogoro]
JKT Ruvu v
Azam FC [Azam Complex, Chamazi]
JKT Oljoro v
Mtibwa Sugar [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Coastal
Union v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Yanga v
Simba [National Stadium, Dar es Salaam]
MSIMAMO VPL 2013/2014.
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Azam FC | 25 | 17 | 8 | 0 | 50 | 15 | 35 | 59 |
2 | Young Africans | 25 | 16 | 7 | 2 | 60 | 18 | 42 | 55 |
3 | Mbeya City | 25 | 12 | 10 | 3 | 32 | 20 | 12 | 46 |
4 | Simba SC | 25 | 9 | 10 | 6 | 40 | 26 | 14 | 37 |
5 | Kagera Sugar | 25 | 8 | 11 | 6 | 22 | 20 | 2 | 35 |
6 | Ruvu Shooting | 25 | 9 | 8 | 8 | 26 | 32 | -6 | 35 |
7 | JKT Ruvu | 25 | 10 | 1 | 14 | 23 | 39 | -16 | 31 |
8 | Mtibwa Sugar | 25 | 7 | 9 | 9 | 29 | 30 | -1 | 30 |
9 | Coastal Union | 25 | 6 | 11 | 8 | 16 | 19 | -3 | 29 |
10 | Mgambo JKT | 25 | 6 | 8 | 11 | 18 | 34 | -16 | 26 |
11 | Tanzania Prisons | 25 | 5 | 10 | 10 | 25 | 33 | -8 | 25 |
12 | Ashanti United | 25 | 6 | 7 | 12 | 20 | 38 | -18 | 25 |
13 | JKT Oljoro | 25 | 3 | 9 | 13 | 18 | 36 | -18 | 18 |
14 | Rhino Rangers | 25 | 3 | 7 | 15 | 18 | 37 | -19 | 16 |
No comments:
Post a Comment