Klabu ya Azam FC imefanikiwa kuweka rekodi mpya kwa kutwaa ubingwa wa
Tanzania bara kwa mara ya kwanza ambapo iliukosa ubingwa huo mara mbili
mfululizo ikishika nafasi ya pili.
|
RASMI Azam FC wamefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara
msimu wa 2013/2014 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City
FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kwa matokoe hayo, Azam FC wamefikisha pointi 59 kileleni ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote ile, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Baadhi ya Wachezaji wa Mbeya City,
Wakimuandama Mwamuzi wa mechi yao
Na Azama FC waliyolala 2-1,
Jana(April 13,2014)
|
Mbeya City baada ya kuchapwa jana(April 13,2014), wanabakia katika nafasi ya tatu kwa pointi 47 na rasmi wameshajiengua kutafuta nafasi ya tatu kwa sababu hata kama watashinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Mgambo JKT aprili 19,2014, watafikisha pointi 50 ambazo zimepitwa na Yanga SC.
Kwa mazingira hayo, Mbeya City wameshika nafasi ya tatu, Yanga SC ya pili na Azam FC ni mabingwa wapya.
Yanga SC waliokuwa wanafukuziana na Azam FC kuwania ubingwa wameshinda mabao 2-1 dhidi ya JKT Oljoro katika dimba la Shk. Amri Abeid jijini Arusha, lakini ushindi huo haujawasaidia chochote kutokana na ushindi wa Azam FC jana(April 13,2014).
Yanga SC wamefikisha pointi 55, pointi nne nyuma ya Azam FC, huku timu zote zikisaliwa na mechi moja moja mkononi.
Hata kama Yanga SC watashinda mechi ya mwisho Aprili 19,2014, uwanja wa Taifa dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC hawataweza kufikia pointi 59 walizonazo Azam FC.
Mabingwa wapya wa Ligi kuu, Azam FC watafunga pazia dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu ambao kwa asilimia zote wamefanikiwa kukwepa kushuka daraja baada ya ushindi wa bao 1-0 walioupata jana katika dimba la Mkwakwani dhidi ya Coastal Union.
Mechi nyingine muhimu jana(April 13,2014) ilipigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam ambapo Wekundu wa Msimbazi Simba SC waliwakaribisha Wauza Mitumba wa Ilala, Ashanti United.
Mechi hiyo imemalizika kwa kocha Abdallah Kibadeni kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mcroatia wa Simba sc, Dravko Logarusic.
Kwa matokeo hayo, Ashanti United wanapata unafuu wa kusalia ligi kuu, huku wakisubiri mechi ya mwisho dhidi ya Prisons aprili 19 mwaka huu uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Sasa Ashanti wamefikisha mechi 25 na kujikusanyia pointi 25 sawa na Prisons walioshinda mabao 4-3 jana dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, lakini Wajelajela wanakuwa juu yao kutokana na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kwa kutwaa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 1 mkononi, Azam FC imefuta
kuhodhi kwa Ubingwa kwa Vigogo Yanga na Simba tangu Mwaka 2001 ambapo, baada ya
Mtibwa kuutwaa Mwaka 2000 na kuutetea Mwaka 2001, Yanga na Simba zimekuwa
zikipishana kwa kuubeba.
MABINGWA
WALIOPITA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA.
1965 Sunderland (Sasa ni Simba SC)
1966 Sunderland
1967 Cosmopolitan
1968 Young Africans
1969 Young Africans
1970 Young Africans
1971 Young Africans
1972 Young Africans
1973 Simba SC
1974 Young Africans
1975 Mseto SC
1976 Simba SC
1977 Simba SC
1978 Simba SC
1979 Simba SC
1980 Simba SC
1981 Young Africans
1982 Pan Africans
1983 Young Africans
1984 Simba SC
1985 Young Africans
1986 Tukuyu Stars
1987 Young Africans
1988 Coastal Union
1989 Young Africans
1990 Simba SC
1991 Young Africans
1992 Young Africans
1993 Young Africans
1994 Simba SC
1995 Simba SC
1996 Young Africans
1997 Young Africans
1998 Young Africans
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba SC
2002 Young Africans
2003 Simba SC
2004 Simba SC
2005 Young Africans
2006 Young Africans
2007 Simba SC
2007/08 Young Africans
2008/09 Young Africans
2009/2010 Simba SC
2010/2011 Young Africans
2011/2012 Simba SC
2012/2013 Young Africans
No comments:
Post a Comment