Ni maoni ya
pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga mkono serikali mbili
alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo wa serikali tatu.
Tundu Lissu:-
‘Nusu karne ya uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na
hakuwa na mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania
kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi hii ni
haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji kuelezwa ukweli’
Mchungaji
Mtikila:- ‘tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki
hii nchi yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano lilikua utapeli
wa kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari’
Mh Wassira:-
‘Hati ya Muungano ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa
Mwenyekiti ndani ya siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni kutaka
kuvunja muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta mgongano’
‘Katiba ya Zanzibar ndio itabakia kuwa sheria kuu kwa Zanzibar kwa mambo yasiyokua ya
muungano, tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata
matatizo, itapunguzia Wazanzibari fursa’
Ismail
Jussa:- ‘Hoja za historia kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika
mgando, ukiangalia katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua Tanganyika
na kuwepo makamu wawili wa Rais’
‘Mkataba wa muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha
kilichopo ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokua Zanzibar tunasema mengine tukija
huku tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu’
‘Zanzibar tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, katika mfumo wa serikali
mbili Zanzibar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali kuendelea nao’
‘Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni
Rais wa Zanzibar kuondolewa kuwa makamu wa Rais’.
No comments:
Post a Comment