UEFA 2013/2014:-Real Madrid na ushindi finyu wa bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich,Ni katika Nusu Fainali ya Mabingwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 24, 2014

UEFA 2013/2014:-Real Madrid na ushindi finyu wa bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich,Ni katika Nusu Fainali ya Mabingwa.


Real Madrid imeibuka na ushindi wa bao 1-0 katika nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Mabingwa watetezi Bayern Munich katika mechi iliyomalizika usiku huu wa April 23,2014,Jijini Madrid.



Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, wenye Real walipata bao lao katika dakika ya 19, mfungaji akiwa Karim Benzema aliyemalizia krosi ya chini ya Daniel Carvajal.





Baadaye Madrid ilipoteza nafasi za kufunga kupitia Cristiano Ronaldo na Angelo Di Maria huku Bayern wanaonolewa na Pep Guardiola ndiyo wakitawala  mchezo kwa asilimia kubwa kwa kupiga pasi fupi fupi.



Real Madrid sasa itakuwa na kibarua kigumu wiki ijayo ,Jumanne ya April 29, 2014, katika mchezo wa marudiano ikitakiwa kuulinda ushindi huo mwembamba mbele ya mabingwa hao watetezi wa Ulaya.

Hapo jana(April 22,2014)-
Chelsea ililazimishwa sare ya bila kufungana na Atletico Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Vicente Calderon.

Chelsea sasa itahitaji ushindi mwembamba katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Stamford Bridge, London (Jumatano April 30,2014)dhidi ya Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad