AJALI:-Abiria Zaidi ya 31 wajeruhiwa katika Ajali ya Basi mkoani Kilimanjaro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 23, 2014

AJALI:-Abiria Zaidi ya 31 wajeruhiwa katika Ajali ya Basi mkoani Kilimanjaro.


Wananchi wawakiwa wanashuhudia ajali ya Basi la URIO iliotokea leo April 23,2014, jioni katika eneo la KIA ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruliwa.

Picha  chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye  basi hilo la Urio lililopata ajali leo April 23,2014,jioni katika eneo la Kia wilayani Hai  mkoani Kilimanjaro.


Basi aina ya Urio lenye namba za usajili T 137 BCX linalofanya safari zake kutoka mjini Moshi kuelekea  Leguruki mkoani  Arusha leo(April 23, 2014) limepinduka katika eneo la KIA na kujeruhi watu zaidi ya 31.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa Dereva wa basi hilo, alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani.

"Dereva alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuhama barabara, ndipo ilipo anguka gafla  na kubiringita mara tatu hapa yenyewe unavyoiyona tumeigeuza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja wapo wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina.

Habari Na:-Dj sek Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad