UEFA 2013/2014:-Haya ndio Matokeo ya Mechi- Man United v Bayern, Barca v Atletico Madrid-Robo fainali ya kwanza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 01, 2014

UEFA 2013/2014:-Haya ndio Matokeo ya Mechi- Man United v Bayern, Barca v Atletico Madrid-Robo fainali ya kwanza.


Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mabingwa watetezi Bayern Munich katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford mjini Manchster, Uingereza Usiku wa April 01,2014.


Man United walikuwa wa kwanza kupata bao lao dakika ya 58 lilifungwa na Nahodha Nemanja Vidic kwa kichwa cha nyuma akimalizia kona ya Wayne Rooney.


Mabingwa hoa wa Ulaya,Bayan walichomoa bao hilo,kupitia kwa mfungaji Bastian Schweinsteiger aliyemalizia kazi nzuri ya Mario ambapo Kwa matokeo hayo, United sasa inahitaji ushindi katika mchezo wa ugenini Aprili 9, mwaka huu.


Katika mchezo mwingine wa Robo ya michuano hiyo usiku huu(April 01,2014), FC Barcelona ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid Uwanja wa Camp Nou.

Diego Coasta alitangulia kuifungia Madrid dakika ya 56 Gabriel ‘Gabi’ Fernandez Arenas, kabla ya Neymar da Silva Santos Junior kuisawazishia Barca dakika ya 71 pasi ya Andres Iniesta. 

FC Barcelona sasa inahitaji ushindi katika mchezo wa marudiano ugenini Aprili 9, mwaka huu. 

Jumatano Usiku (April 02,2014) kutakuwa na  Mechi mbili ambapo huko Santiago Bernabeu, Jijini Madrid, Real Madrid wataivaa Borussia Dortmund na huko Parc des Princes, Jijini Paris, France, Paris Saint-Germain itakumbana na Chelsea.

UEFA CHAMPIONZ LIGI ROBO FAINALI  

Jumanne Aprili 1,2014.

Barcelona 1 v 1 Atletico Madrid
Manchester United 1 v 1 Bayern Munich

Jumatano Aprili 2,2014.

Real Madrid v Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain v Chelsea

Marudiano,Jumanne Aprili 8,2014.


[Saa 3 Dak 45 Usiku]

Chelsea v Paris Saint-Germain
Borussia Dortmund v Real Madrid

Jumatano Aprili 9,2014.

Bayern Munich v Manchester United
Atletico Madrid v Barcelona

-Droo ya Nusu Fainali:- 11 Aprili,2014.


-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili,2014.


-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad