![]() |
|
Wasailiwa
walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:-
|
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa 1:00 kabla
ya muda wa mtihani wa mchujo kuanza.
2. Kwa wale
wasiokuwa na mtihani wa mchujo usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na
utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Kuja na
kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura,
kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Kuja na
Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada,
Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”,
“Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila
msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa
chakula, usafiri na malazi.
8. Kila
msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9. Kila
msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10. Kwa wale
waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa
na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale
ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao
hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
12. Kada
zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na
tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.
KUTAZAMA
JINA LAKO FUNGUA HAPA>>>>>http://www.scribd.com/doc/220689798/Tangazo-La-Usaili-April-2014






No comments:
Post a Comment