Wakati
mjadala kuhusu sura ya kwanza na sita kwenye Bunge Maalumu ukielekea ukingoni,
baadhi ya wajumbe wametoleana kauli ambazo zimesababisha kutoelewana.
Kiini cha
hayo ni aina ya muundo wa Muungano unaotakiwa kuwekwa kwenye Katiba Mpya, suala
ambalo wajumbe badala ya kulijadili kwa hoja, wakaishia kushambuliana kwa
maneno.
Kwa muda
mrefu hali haikuwa shwari, kwani dakika 10 zilizotengwa kwa ajili ya mjumbe kuchangia
mjadala, wengi walizitumia kumaliza hasira dhidi ya wenzao au kuponda mchango
uliotolewa awali na mjumbe mwingine.
Hebu tuone
mifano ya kauli zilizoacha majeraha bungeni hivi karibuni.
![]() |
| Waziri William Lukuvi. |
Kauli ya
Lukuvi
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema
Chama cha Wananchi (CUF) ni sehemu ya kikundi cha Uamsho kinachoisumbua
Serikali ya Zanzibar.
Lukuvi
akaenda mbali zaidi na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif
Sharifu Hamad, ni mchochezi ambaye amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvuruga
Muungano na kudai anastahili kupelekwa katika Mahakama ya Uhalifu wa Makosa ya
Jinai The Hague - Uholanzi.
Kauli hii
inaweza kuonekana kama njia ya kuzuia wananchi wasikiamini Chama cha CUF katika
mchakato wa Katiba Mpya.
Profesa
Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti
wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihitimisha hotuba kwa mujibu wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), akalifananisha Bunge Maalumu na kundi la
Intarahamwe.
Kundi hilo
ni lile lililoendesha mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994.
Felix
Mkosamali
Mbunge wa
Muhambwe, Felix Mkosamali alisema Rais Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, ni viongozi vigeugeu ambao hawawezi
kufikisha nchi mahali popote.
Kiumri
Mkosamali ni mdogo kuliko wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Alisema nchi
haiwezi kuendelea kuongozwa na viongozi vigeugeu, kauli ambayo imewachukiza
zaidi viongozi wa Serikali.
Vijembe
kutoka Zanzibar
Mwakilishi
wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa alieleza kuwa baadhi ya wajumbe wenzake kutoka
Zanzibar ‘wameufyata’, akimaanisha hawakutetea walichokubaliana kabla ya kufika
Dodoma.
Hata hivyo,
naye akapigwa kombora na Asha Bakari Makame, ambaye alitafsiri kuufyata kuwa ni
sawa na mtu mwenye busha.
Akaeleza
bungeni kuwa mwenendo wa maisha ya Jussa unatia shaka kwa sababu ana umri
mkubwa, lakini hajaoa wala hana watoto.
Masauni na
Kupindua Serikali
Hamad
Masauni Yussuf alituhumu wanaopinga Serikali mbili kuwa ndiyo wamekuwa na mbio
za kutaka kupindua Serikali.
![]() |
| Wabunge Maalumu. |
Pia alisema
kauli za wajumbe hao zinaifafanisha hati ya Muungano na barua ya mapenzi,
akaeleza bungeni kuwa watakaporejea Zanzibar watawahangaikia watu hao hata kama
watajificha shimoni.
Omary Ali
Shehe
Huyu naye
akaibuka na kauli tata akisema, “Wanaolazimisha serikali mbili mpaka kutokwa
povu mdomoni ni wanafiki na wasaka tonge.”
Mrema na
Sanya
Mbunge wa
Vunjo, Augustino Mrema alishauri watu wasikubaliane na Serikali tatu kwa sababu
hali ya usalama ya taifa siyo shwari, hasa kwa Zanzibar aliyodai inanyemelewa.
Mohammad
Sanya
Mkongwe huyu
wa siasa za upinzani Zanzibar akaita wawekezaji kutoka Tanzania Bara waliopo
visiwani humo kuwa ni wauza karanga na dawa za mende. Alitaka Zanzibar iachwe
ijijenge kwa kiwango cha kuwa Dubai na Hong Kong nyingine.
Diana
Chilolo
Anasema ana
shaka juu ya Tundu Lissu kufunga ndoa na wajumbe kutoka Zanzibar na kwamba
anashangaa ndoa hiyo ni ya aina gani.
Lissu na
Askofu
Tundu Lissu
alisema kukosoa yaliyofanywa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, siyo dhambi kwa
kuwa hakuwa Malaika wala Mungu hivyo alipokosea lazima akosolewe hadharani.
Chanzo:-Mwananchi.








No comments:
Post a Comment