AJALI YA BASI LA LUHUYE:-Idadi ya waliokufa yaongezeka…..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 23, 2014

AJALI YA BASI LA LUHUYE:-Idadi ya waliokufa yaongezeka…..’’


Dr. Derick David ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dharura Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza..Picha Na:-Gsengo.

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na  ajali ya basi la kampuni ya Luhuye lililo pata ajali April 21,2014,katika eneo la Masanza Kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu majira ya asubuhi likitokea wilayani Tarime Mkoani Mara Kwenda Mwanza inatajwa kuongezeka kutoka ile ya awali 11 na sasa kufikia 16.

Kwa mujibu wa Dr. Derick David ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dharura Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza amesema kuwa jana(April 22,2014) idara yake ilipokea watu 35, kati yao watu wawili walifariki dunia wakati wakipewa matibabu, miili ya watu wengine wawili waliletwa ikiwa tayari imepoteza uhai wakati wa harakati za kufikishwa hospitali hapo na mmoja ameongezeka akiwa kwenye matibabu hivyo kufanya ongezeko la watu watano na kufikisha idadi ya watu 16 hadi sasa.



Ongezeko la majeruhi hospitalini hapo limesababisha msongamano kiasi cha kusababisha wagonjwa kulazwa wawili wawili kwenye Kitanda kimoja.

Huku wakisimulia kilichotokea na hatimaye kusababisha ajali hiyo, majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza wamesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi na Majeruhi wa ajali ya basi Peter Funga naye amelaumu vitendo vya baadhi ya madereva kutozingatia kanuni na sheria zinazowaongoza barabarani hata kusababisha ajali...Picha Na:-Gsengo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad