PICHA:-Muonekano wa matukio ya Ligi ya Makoye-2014-kata ya Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera na Benaco Stars kuibuka Mabingwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 01, 2014

PICHA:-Muonekano wa matukio ya Ligi ya Makoye-2014-kata ya Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera na Benaco Stars kuibuka Mabingwa.


Kikosi cha Timu ya Benaco Stars,ambao ni Mabingwa wa kwanza wa Ligi ya Makoye 2014 katika picha ya pamoja katika uwanja wa Benaco-Ngara,Kagera na kilifanikiwa kubeba Ubingwa huo baada ya kumfunga Kumunazi FC bao 2-1 katika mchezo wa fainali  March 30,2014- Jumapili .



Kikosi cha Timu ya Kumunazi FC,licha ya kucheza soka safi na la kuvutia lakini kilikubali kupoteza mchezo wao huo wa fainali dhidi ya Benaco Stars March 30,2014 mjini Benaco.



Waamuzi wa mchezo huo wa fainali kati ya Benaco Stars na Kumunazi FC walikuwa ni Ramadhani Makule,Rwegasira Kashunja na Abdul Mwandik.



Diwani wa kata ya Kasulo  Philbert Kiiza alikua mgeni rasmi na alipata fursa ya kuzikagua timu zote mbili na kuwataka kucheza mchezo safi kwa kuacha fujo na jazi sambamba na kuzingatia fair play.



Wanne kutoka kushoto ni mwakilishi wa Mdhamini wa Ligi ya Makoye-2014 kata ya Kasulo, Costantine Morandi amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu kwa kuchezwa kila Mwaka katani humo.


Mgeni rasmi Diwani Philbert Kiiza akizungumza na timu zote mbili mara baada ya kuzikagua.


Mashabiki mablimbali wakifatilia mchezo huo wa fainali katika uwanja wa Benaco ambapo Benaco Stars ilifanikiwa kuibuka Bingwa wa Ligi ya Makoye 2014,kwa ushindi wa bao 2-1.



Muonekano wa uwanja wa Benaco licha ya timu kucheza soka safi na la kuvutia ,ila uwanja uliwaathiri wachezaji kwa kujaa tope na kuteleza kwa sababu ya mvua kunyesha kabla ya mchezo.



Benchi la Ufundi la Timu ya Benaco Stars na wapili ni kocha wa Benaco FC- James Elieza.


Mwakilishi wa Ligi ya Makoye -2014, Costantine Morandi akifatilia mchezo huo wa fainali March 30,2014,kati ya Benaco Stars na kumunazi FC katika uwanja wa Benaco-Ngara ,Kagera.


Diwania wa kata ya Kasulo na mgeni rasmi katika fainali hiyo Philbert Kiiza katikati na kulia kwake ni Diwani wa Kata ya Rusumo ,Wilbrord Bambara wakitabasamu na kufatilia mchezo huo wa fainali March 30,2014,kati ya Benaco Stars na kumunazi FC katika uwanja wa Benaco-Ngara ,Kagera.


Katikati ni Afisa mtendaji wa Kata ya Kasulo,wilayani Ngara mkoani Kagera ,Dauson Miburo akiwa na baadhi ya wananchi na wadau wa michezo wakati wa fainali hiyo  March 30,2014, katika uwanja wa Benaco-Ngara ,Kagera.




Zawadi ya Mabingwa wa Ligi ya Makoye -2014,ambao ni Benaco Stars  waliondoka na  Ng'ombe mnyama mwenye thamani ya shilingi za kitanzania Laki 5 na elfu 40 huku mshindi wa Pili-Kumunazi FC akiondoka na shilingi Laki Moja.



Katika fainali hiyo ulinzi pia wakutosha uliimarishwa na askari mgambo na walinzi wa Polisi Jamii.
Magoli 2 ya wachezaji Silvester John na Jacksoni John yalitosha kuwapa Ubingwa wa kwanza msimu huu Timu ya Benaco Stars,baada ya hapo March 30,2014- Jumapili kufanikiwa kuifunga timu ngumu ya Kumunazi FC bao 2-1.

Mchezo huo uliokuwa wa fainali ya Ligi ya Makoye kwa timu za kata ya Kasulo,wilayani Ngara mkoani Kagera,ulichezwa katika uwanja wa Benaco na kushuhudiwa na idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka toka katani humo.

Wakicheza soka safi na la kuvutia ,licha ya uwanja kuwa na tope na kuteleza kwa sababu ya mvua kunyesha kabla ya mchezo,Kumunazi FC walijikuta wakifungwa bao la kwanza kwa njia ya Penati iliyofungwa na Jacksoni Joni baada ya mchezaji wa Kumunazi ambae alikuwa wa mwisho kumkwatua rafu mchezaji wa Benaco FC katika eneo la 18,huku goli la kufutia machozi la Kumunazi FC likifungwa na Ramadhani Shija.

Baada ya kumalizika mchezo ,kocha wa Benaco FC- James Elieza licha ya kufurahia Ubingwa huo alitoa ushauri kwa kamati ya Mashindano ya Ligi ya Makoye,kuboresha mashindano yajayo kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza za kisheria na Wamuuzi na kuzingatia kanuni za mashindano.


Kwa upande wake Nahodha wa Timu ya Kumunazi FC-JUMA MUSSA licha ya kusifia mchezo huo wa fainali kuwa mzuri lakini hakusita kuwatupia lawama mwamuzi wa kati wa mchezo huo Ramadhani Makule,Rwegasira Kashunja na Abdul Mwandike kuwa hawakumudu vyema sheria 17 zinazotawala mchezo wa soka.

Mshindi katika fainali hiyo ya Ligi ya Makoye –Mfungaji bora alikuwa ni Ramadhani Shija kwa kufunga magoli 9 toka timu ya Kumunazi FC -10,000,Timu yenye nidhamu Kisabule FC-10,000-Washindi wa 3-Rusumo Sekondari-50,000-washindi wa pili Kumunazi FC 100,000 na Mabingwa Benaco Starz  waliondoka na zawadi ya Ng'ombe mnyama mwenye thamani ya shilingi za kitanzania Laki 5 na elfu 40 zawadi ambayo walikabidhiwa na Diwani wa kata ya Kasulo  Philbert Kiiza na kuwataka kuitunza zawadi hiyo ili iwalete manufaa na kupiga hatua kiuchumi.


Awali kwa niaba ya mdhamini wa Ligi ya Makoye-Athumani Makoye-mwakilishi wake Costantine Morandi amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu kwa kuchezwa kila Mwaka katani humo.

Ligi hiyo ilifadhiriwa na Athumani Makoye pamoja na mambo mengine alitoa vifaa vya michezo kwa timu 8 zilizoshiriki vyevye thamani ya shilingi Milioni 4 na Laki 4 na elfu 80.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad