Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku
askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo
la tukio.
|
Basi aina ya Coster linalofanya safari zake Kibwabwa ,Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. |
Zaidi ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali
iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya
Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya
saa saba mchana wa siku ya jana (April 22,2014).
Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo,
eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo
imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani
Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus
hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina
ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na
waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi
wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi
nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
No comments:
Post a Comment