MAWASILIANO:-Makampuni ya simu Tanzania yaweka saini mkataba wa makubaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini (UCSAF). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 23, 2014

MAWASILIANO:-Makampuni ya simu Tanzania yaweka saini mkataba wa makubaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini (UCSAF).

Kutoka kulia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga wakitia saini makubaliano yanayayawezesha makampuni ya simu kupokea ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo pemebezoni na miji kadiri walivyoomba. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye kata 73 kati ya hizo 37 kupitia ruzuku YA UCSA.

Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania wa kwanza kulia na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura (katikati) wakipitia kwa umakini mikataba kati ya makampuni yao na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inazoziwezesha kampuni hizo kupokea ruzuku kusaidia usamabzaji wa huduma za mawasiliano ya simu vijijini. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter Ulanga akitia saini makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye kata 73za vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku ya UCSAF

Mkuu wa Idara ya Sheria wa Vodacom Ngayama Matongo akimuongoza Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Georgia Mutagahywa (aliyeketi) kutia saini mkataba wa makubaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini kupitia ruzuku ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam. Wa pili kulia aliyesimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akishuhudia. Vodacom kupitia mfuko huo itafikisha huduma kwenye kata 73 za pembezoni mwa miji na yenyewe ikiahidi kufikisha huduma kwenye kata 37 za pembezoni kwa gharama zake ili kuwawezesha watanzania waishio vijijini kuunganishwa kwenye mtandao wa huduma za simu za mkononi.

 Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa kulia akibadilishana nyaraka za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura zinazohusiha upokeaji wa ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter Ulanga akisainia makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma kwenye kata 73 zilizopo vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku hiyo. Wa pili kulia waliosimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza kwa makini Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa (kulia) muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya utiaji saini mikataba ya usambazaji huduma za mawasiliano ya simu za mkononi maeneo ya vijijini kati ya makampuni ya simu na Mfuko wa Wamasiliano kwa Wote - (UCSAF) jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Beatrice Bandawe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad