Mtoto Samir
anayekadiriwa kuwa na umri wmiaka minne hadi mitano mkazi wa mtaa wa Langoni
katika manispaa ya Moshi, amejikuta katika wakati mgumu kutokana na tabia ya
bibi yake kumfunga kamba katika mguu wake kwa lengo la kumzuia asiende kucheza
mbali na nyumbani kwao.
Tukio hilo
limetokea hivi karibuni katika eneo hilo ambapo bibi huyo ambaye jina lake
halikufahamika mara moja alikutwa akiwa amemfunga kamba ya kudu mjukuu wake
huyo katika mguu wa kushoto huku sehemu nyingine ikiwa imefungwa katika chuma
kizito.
Kwa mujibu
wa majirani walisema bibi huyo amekuwa akimfunga mtoto huyo mara kwa mara kwa
zaidi ya nusu saa hasa nyakati ambazo bibi huyo amekuwa akifanya shughuli zake
za usafi wa ndani pamoja na kufua.
Wakizungumza
kwa sharti la kutotajwa majina,majirani hao wamesema imekuwa ni kawaida kwa
bibi huyo ambaye anaishi na wajukuu zake kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo
huku akimzuia kucheza na wenzake wa nyumba za jirani.
“Sisi hiyo
hali mbona tumeizoea mara kwa mara Samir akienda kucheza na wenzake huko
mtaani,bibi yake akimkuta huko anamkamata na kisha kumfunga kwenye hilo chuma
lililoko hapo mlangoni kwa zaidi hata ya nusu saa”alisema mmoja wa majirani.
Akizungumza
tukio hilo Bibi huyo ambaye anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 60 alikiri
kumfunga mtotot huyo kwa madai kuwa amekuwa mtundu kupita kiasi na kwamba
ametumia mbinu hiyo ili kumdhibiti asitoroke nyumbani.
“Hapa
nyumbani naishi na wajukuu zangu ,wengine wako mashuleni na wengine wako kazini
ambao ni wazazi wa huyu Samir,mmoja anafanya kazi Arusha,mwingine yuko hapo
mjini(Moshi)sasa sina mtu wa kunisadia kumwangalia huyu mtoto”alisema Bibi
huyo.
Alisema
analazimika kumfunga kamba mtoto Samir kutokana na kuwa na tabia ya kwenda
kuzurura katika nyumba za watu huku wakati mwingine huenda kucheza mbali na
nyumbani jambo ambalo humpa shida kumpata kwa urahisi.
“Wakati
mwingine nashikwa na hasira kumpiga siwezi hivyo naamua kumfunga kamba hapa
mlangoni…watu wote si wazuri kumruhusu kuingia kila nyumba huko atafundishwa
mambo mabaya ndio sababu nafanya hivi.”alisema Bibi huyo.
Mmoja wa
wazazi walioshuhudia tukio hilo walisema wazazi wengi wamekuwa wakikosea
kuwaacha watoto wao walelewe na bibi zao hali inayochangia kuwepo kwa vitendo
vya ukiukaji wa hali ya watoto na kibinadamu kama ilivyotokea kwa mtoto huyo.
“Wazazi
tumekuwa bize sana na shughuli za utafutaji ,hali hii inapelekea majukumu ya
kulea watoto kuiacha kwa wasichana wa kazi na hata mama zetu kama ilivyo kwa
familia hii ,sasa suala hili pia wakati mwingine linachangia makuzi mabovu kwa
watoto”alisema Juma Nzota.


.jpg)



No comments:
Post a Comment