![]() |
Mpiga gitaa
wa bendi ya Double M Sound-Ally Akida aka Tetenasi ya Geneva akiungurumisha
Jana (April 21,2014) wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika ukumbi wa New Happy mjini Ngara.
|
Mkurugenzi
wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Double M Sound Mwinjuma Muumini ameeleza namna
alivyoupokea msiba wa Gwiji wa Muziki wa Dansi Nchini Muhidin Maalim Gurumo
aliyefariki hivi karibuni jijini Dar es salaam na amesema kuwa
kilichomsikitisha zaidi ni kuona Mzee Gurumo amefariki kabla hawajatimiza
malengo yao ya kufanya kazi za pamoja kutokana na kukabiliwa na maradhi
mfululizo.
Katika
mahojiano na mwenzangu Seif Omary Upupu, Mwinjuma amesema Mzee Gurumo alikuwa
akiwasaidia wanamuziki wengi katika ushauri wa masuala mbalimbaliu ya Kimuziki.
Pia
akazungumzia ushiriki katika Tuzo za Muziki za Kilimanjaro ambzo zinahusisha
wanamuziki wa aina mbalimbali, amewaomba Watanzania wote kumpigia kura katika
Tuzo za mwaka za Kilimanjaro Music Award’s kwa kuchagua wimbo wake bora wa
Kiswahili wa SHAMBA LA BIBI kwa kuandika (SMS AC2 kisha tuma namba 15440).
Baada ya
miaka kadhaa ya ukimya wa Bendi yake ya Double M Sound aliyodai ilikufa kifo
cha kawaida kutokana na uchakavu wa vifaa, Muumini amelazimika kukimbia jijini
Dar Es Salaam na kuweka maskani mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako ameifufua
Bendi hiyo na kuahidi makubwa zaidi katika Bendi yake.
No comments:
Post a Comment