Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha
kuwa ajali zabarabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu wasiokuwa na
hatia.
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya ajali hiyo ambayo nimejulishwa
kuwa imetokea katika Kijiji cha Itwimila katika Wilaya ya Busega katika Mkoa
wako wa Simiyu wakati basi lililokuwa linasafiri kutoka Tarime, Mkoa wa Mara
kwenda Mwanza kupitia Simiyu lilipoacha njia na kugonga nyumba kabla ya
kupinduka.”
Amesema Rais Kikwete: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi na najiunga
nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu.
Aidha, kupitia
kwako, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia zote ambazo zimepoteza
wapendwa wao katika ajali hiyo. Naungana nao katika kuomboleza wapendwa wao.
Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aziweke peponi roho za marehemu.”
Rais Kikwete vile vile ametoa pole kwa wote ambao wameumia katika ajali
hiyo, akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea
maendeleo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014
No comments:
Post a Comment