Treni hiyo
ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu baadhi wakiwa wamekaa juu ya treni.
|
Takriban
watu 63 wamefariki baada ya treni iliyokuwa imebeba abiria kupoteza mwelekeo
Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Msemaji wa
serikali Lambert Mende alisema kuwa polisi wanahofia kuwa idadi ya watu
waliofariki huenda ikaongezeka. Pia alisema kuwa polisi watafanya uchunguzi
kubaini chanzo cha ajali.
Ajali hiyo
ilitokea karibu na eneo la Kamina katika mkoa wenye utajiri wa madini wa
Katanga.
Treni hiyo
ilikuwa imebeba idadi kubwa ya watu kupindukia wengine wakiwa wameketi juu ya
treni yenyewe.
Waziri wa
mambo ya ndani katika mkoa huo Jean Marie Dikanga Kazadi, aliambia BBC
kuwadereva wa treni hiyo alikuwa anaiendesha kwa kasi .
Watu 80
walijeruhiwa vibaya huku wengine saba wakiwa bado wamekwama ndani ya treni
vifusi.
Treni
ilianguka Jumanne (April 22,2014) asubuhi lakini waokozi waliweza tu kuwasili nyakati za jioni.
Sehemu kubwa
ya njia ya reli ya DRC, imesalia katika hali yake tangu enzi za ukoloni na ni
nadra kufanyiwa ukarabati.
Treni hiyo
ilianguka wakati dereva alipokuwa anajaribu kupunguza kasi.
Habari Na:-BBC-Swahili.
No comments:
Post a Comment