Watu 29
wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali mbili tofauti katika eneo la Mikese na
Mkambalani,barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam,moja ikihusisha Basi la
Nganga likitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya na Basi la Sumry likitokea
Tunduma ambalo limegongana uso kwa uso na coster likijaribu kulipita gari
jingine lililokuwa mbele jana March 31,2014.
Ajali ya
kwanza imetokea majira ya saa 2 usiku katika eneo la Mkambalani, ikihusisha
basi la kampuni ya Sumry likitokea tunduma kwenda Dar es salaam ambalo
limegongana uso kwa uso na bas dogo la abiria aina ya costa lililokuwa
kikitokea dar es salaam kuelekea mbeya na kusababishabmjeruhi 15,na chanzo cha
ajali kikidaiwa ni dereva wa sumry kujaribu kulipita gari lililokuwa mbele, na
kukutana uso kwa uso na costa, huku ,ajali ya basi la nganga ikitokea
majira ya saa 3 na nusu asubuhi, katika eneo la miembeni mikese,baada ya kupata
pancha kwa tairi ya mbele kulia na kusababisha majeruhi 14 na majeruhi hao
waepelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwamatibabu.
Aidha
mashuhuda wa ajali hiyo waliokutwa eneo la tukio nao wamezungumza kuhusiana na
ajali hizo.
Mganga wa
zamu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,Dk Alex Makala, amesema
majeruhi wengine wametibiwa na kuruhusiwa na kwamba wamebaki majeruhi 14
wakiwemo 12 wa Sumry na wawili wa Nganga,na wengi wamepata majeraha madogo
madogo na wanaendelea vyema na matibabu,huku kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro
faustine shilogile akizungumza kwa njia ya simu, amesema dereva wa basi
la sumry mhina mohamed(39)mkazi wa mbeya amejisalimisha polisi majira ya
asubuhi baada ya kukimbia kufuatia ajali hiyo, huku dereva wa basi
la Nganga Alex Elia(49) mkazi wa Misufini Morogoro akiishikiliwa kwa mahojiano
zaidi.
Source:-Itv-Habari.






No comments:
Post a Comment