AFCON 2015:-Droo ya Kufuzu kwa kombe la Mataifa Bingwa Barani Afrika mwakani yatangazwa-Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi zikianzia mechi za Mchujo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 28, 2014

AFCON 2015:-Droo ya Kufuzu kwa kombe la Mataifa Bingwa Barani Afrika mwakani yatangazwa-Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi zikianzia mechi za Mchujo.



Droo ya Kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa Barani Afrika mwakani { AFCON 2015 } imefanyika huko Jijini Cairo nchini Misri huku timu zote za kanda ya Afrika Mashariki zikipangwa kucheza katika mechi za mchujo kabla ya kushiriki mechi za kufuzu.
Kenya itachuana dhidi ya Visiwa vya Comoro ,Tanzania itapambane na Zimbabwe, Uganda dhidi ya Madagascar huku Rwanda ikivaana na Libya.

Burundi kwa upande wake itachuana dhidi ya Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikipambana na Namibia.

Raundi ya Kwanza 

  • Liberia  v/s  Lesotho
  • Kenya  v/s  Comoros Islands
  • Madagascar  v/s  Uganda
  • Mauritania  v/s  Equatorial Guinea
  • Namibia  v/s  Congo
  • Libya  v/s  Rwanda
  • Burundi  v/s  Botswana
  • Central African Republic  v/s  Guinea Bissau
  • Swaziland  v/s  Sierra Leone
  • Gambia  v/s  Seychelles
  • Sao Tome e Principe v/s  Benin
  • Malawi  v/s  Chad
  • Tanzania  v/s  Zimbabwe
  • Mozambique  v/s  South Sudan
Baada ya kushiriki mkondo wa kwanza wa maondoano, mataifa hayo tena yatalazimika kuchuana miongoni mwao ilikufuzu kwa awamu ya pili.

Mshindi wa mkondo huo wa pili ndio watakaojumuishwa katika makundi saba yaliyotangazwa na CAF.

Raundi ya Pili.

Liberia au Lesotho  v/S  Kenya au Comoros Islands

Madagascar au Uganda  v/s  Mauritania au Equatorial Guinea

Namibia au Congo  v/s  Libya au Rwanda

Burundi  au Botswana  v/s  CAR au Guinea Bissau

Swaziland  au  Sierra Leone  v/s  Gambia au Seychelles

Sao Tome e Principe au Benin  v/s  Malawi au Chad

Tanzania au  Zimbabwe  v/s  Msumbiji au Sudan kusini

Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa kati ya tarehe 6-18 Mei.

Mechi za marudio zitasakatwa wikiendi ya tarehe 30-31 Mei hadi Juni Mosi .

Katika mechi zitakazoibua hisia ni pamoja na Mabingwa watetezi Nigeria ambao wamepangwa kuvaana na Afrika Kusini.

Mahasimu wa jadi kaskazini mwa Afrika Tunisia na Misri watakwaruzana huku Ghana ikitoana kijasho na Togo.

Aidha Ivory Coast itafungua kampeini yake ya kufuzu kwa dimba hilo lenye hadhi barani dhidi ya mahasimu wao wakuu Cameroon.

Droo ya Makundi.

Kundi A :

Nigeria,
Sudan,
South Africa
{Namibia vs Congo Brazzaville/Libya vs Rwanda}

Kundi B

Mali,
Ethiopia,
Algeria
{ Sao Tome e Principe vs Benin/Malawi vs Chad}

Kundi C

Burkina Faso,
Gabon,
Angola
{ Liberia vs Lesotho/Kenya vs Comoros Islands}

Kundi D:
Ivory Coast,
Democratic Republic of Congo,
Cameroon
{ Swaziland vs Sierra Leone/Gambia vs. Seychelles}

Kundi E:
Ghana,
Guinea,
Togo
{Madagascar vs Uganda/Mauritania vs Equatorial Guinea}

Group F:
Zambia,
Niger,
Cape Verde Islands
{ Tanzania vs Zimbabwe/Mozambique vs South Sudan}

Kundi G:
Tunisia,
Senegal,
Egypt
{ Burundi vs Botswana/ Central African Republic vs Guinea Bissau}

Mechi za makundi zitaandaliwa kati ya tarehe 5-6 Septemba na tarehe 10 Septemba.

Mkondo wa pili utaandaliwa kati ya tarehe 14-15 November na 19 November.

Washindi wawili katika kila kundi watajiunga na wenyeji Morocco mwakani kwenye kipute cha kuwania taji la taifa bingwa barani Afrika 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad