WITO:-Waandishi wa Habari watakiwa kutumia Uhuru wa Habari kuepuka kuandika habari za kushusha hadhi na uchohezi nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 16, 2014

WITO:-Waandishi wa Habari watakiwa kutumia Uhuru wa Habari kuepuka kuandika habari za kushusha hadhi na uchohezi nchini.


Waandishi wa Habari wakiwa jijini Mwanza kwenye Mafunzo Elekezi kwa Waandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Kanda ya Ziwa leo March 16,2014.


Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye Mafunzo elekezi kwa Waandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Kanda ya Ziwa,wakimsikiliza Human Resource wa Mwananchi ,Aika Massawe akitoa mada ya uadilifu kiutendaji.

Kutoka kushoto ni Bw.Theophil Makunga na Bw.Midraji Ibrahimu(kulia) ambao ni Wahariri wa Habari wa Gazeti la Mwananchi-Kanda ya Ziwa.

Meneja Utawala na Sheria wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd Bi Doris Maliale ambapo pamoja na Mambo mengine amewataka Waandishi wa Habari kutumia Uhuru wa Habari kuepuka kuandika habari za kushusha hadhi za watu na za uchohezi bila kuwa na uthibitisho kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na maadili ya taaluma.

Wanahabari wametakiwa kutumia uzalendo wa uhuru wa habari kwa kuepuka kuandika habari za kushusha hadhi za watu pamoja a uchohezi na kusababisha uvunifu wa sheria endapo hakutakuwa na ushahidi wa kutosha  kuhusu taarifa zao.

Meneja utawala na sheria wa Mwananchi Communication Ltd Doris Maliale alisema hayo leo March 16,2014, katika mafunzo elekezi kwa wanahabari wagazeti hilo  kanda ya ziwa na kwamba habari zenye migogoro huleta hasara kwa Taasisi ama  kampuni.

Alisema madhara makubwa yanapotokea hukumba watumishi mbalimbali wa  taasisi kuanzia mwandishi hadi mchapishaji habari ambapo rasimali fedha hutumika na kuharibu mipango ya uzalishaji na kuibua migogoro ndani ya jamii.

Alisema katika kutumia maadili ya uandishi wajihadhari na kuwatishia watuhumiwa wa mambo mbalimbali kwenye taasisi na lazima kukusanywe ushahidi wa pande mbili na kujiridhisha na ukweli utakaokuwa umetolewa.

“Uandishi unaweza kumpandisha mtu hadhi  yake ama kuishusha hivyo kunahitaji uangalifu katika kufanya kazi kwenye mazingira ya habari ikiwa ni pamoja na kubainisha source husika kuliko kutaja kundi la watu ama kampuni”.Alisema.

Kwa upande wake mhariri mtendaji Theophil Makunga alisema kampuni ya MCL imekujipanua kwa kuingia ubia na kampuni ya  Jamana katika kuchapa gazeti hilo na kusambaza nakala kwa wasomaji wengi kanda ya ziwa ifikapo April mwaka huu. 

Alisema mpango wa kuanza kuchapicha nakala hizo tayari umekamilika kinachosubiliwa ni Tanesco kusambaza umeme kwenye kiwanda cha uchapaji na magazeti yatakayochapishwa ni mwananchi mwanaspoti na the Citzen.

“Tumejipanga kuhudumia wananchi wetu kupata habari kwa wakati na mipango inapanuka mwaka jana tulianzisha breacking news na tunatarajia hata kuwa na Tv na radio kufikia mwakani na kuingia zaidi katika website”.Alisema Makunga.

Aidha  mhariri  wa habari za kanda ya ziwa Midraji Ibrahimu alisisitiza wanahabari kuhakikisha wanafika kwenye eneo la tukio na kutuma habari zenye uhakika ili  jamii inawaamini na wao kufanya kazi katika mazingira ya usalama.

Katika hatua nyingine ,Kampuni ya gazeti la Mwananchi limepanua wigo wa kuandika habari kutoka kanda ya ziwa kwa kutoa vipaumbele sita ili wananchi wapate habari zinazoelezea changamoto na fursa katika sekta za uzalishaji mali.

Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi Bw Bakari Machumu amesema hayo leo kwa wanahabari  walioko kanda ya ziwa wakati wa semina elekezi juu ya mipango ya upanuzi na  utoaji huduma kwa wananchi wanaotakiwa kusoma gazeti hilo.

Bw Machumu amesema kuwa katika habari za kanda ya ziwa kipaumbele ni  katika sekta ya  uchimbaji madini ,kilimo , uvuvi,siasa ,biashara na utalii pamoja na manufaa yake katika ujasiliamali ndani ya jumuia ya afrika Mashariki.

Hata Hivyo mhariri wa habari za kanda ya ziwa Midraji ibrahimu amesema Habari yoyote itakayopelekwa mwananchi (MCL) lazima mwandishi awe amefika eneo la tukio na kujiridhisha na mambo yanayotukia na kukusanya ushahidi wa kutosha.

Habari Na:- Shaaban Ndyamukama
MWANZA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad