Tazama Picha ya bidhaa bandia zilizokamatwa katika wilaya za Kibondo na Kakonko Mkoani Kigoma na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kanda ya kati na kuziteketeza - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 16, 2014

Tazama Picha ya bidhaa bandia zilizokamatwa katika wilaya za Kibondo na Kakonko Mkoani Kigoma na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kanda ya kati na kuziteketeza


Ukaguzi huo uliofanywa hivi karibuni katika wilaya za Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma  na TFDA kanda ya kati ,ulilenga kuangalia utekelezaji wa sheria ya chakula dawa na vipodozi namba moja ya mwaka 2003 katika udhibiti wa ubora usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula dawa  vipodozi na vifaa tiba .

Bidhaa hizo zimekamatwa kufuatia ukaguzi uliofanywa na TFDA kwenye maduka 72 ya wilaya ya Kibondo na mengine matano kwenye wilaya ya Kakonko.



Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kanda ya kati iliziteketeza bidhaa hizo  bandia zilizokamatwa katika wilaya za Kibondo na Kakonko Mkoani Kigoma.



Kukamatwa kwa Bidhaa hizo zisizofaa ziliteketezwa kama unavyojionea ambapo Mmoja wa wafanyabiashara wilayani Kibondo Bw.Musa Hamisi ameitaka mamlaka ya chakula na dawa kudhibiti wafanyabiashara wakubwa kwa kuwa wao ndio husambaza bidhaa zisizo na ubora kwa wafanya biashara wadogo.

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA Tanzania,Kanda ya kati imeteketeza tani moja na nusu ya  bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu bidhaa ambazo zimekusanywa kutoka maduka mbali mbali yaliyoko katika wilaya za Kakonko na Kibondo mkoani Kigoma.

Mkaguzi wa chakula kutoka mamlaka ya chakula na dawa TFDA ,Kanda ya kati Bw. Abel Deule  amesema kuwa ofisi ya mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya kati katika kutekeleza mpango kazi wake kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2013/14 imefanya ukaguzi katika halmashauri za wilaya ya Kibondo na Kakonko kwa kushirikiana na Ofisi za Waganga wakuu wa Halmashauri hiz.

Amesema kuwa uelewa mdogo wa wafanyabiashara kuhusu matakwa ya sheria ya chakula, dawa na vipodozi ndio unaosababisha washindwe kufuatilia ubora na usalama wa bidhaa.

Aidha Bw Deule amesema kuwa lengo la ukaguzi huo ni kuangalia hali ya usajili na vibali vya biashara, uwepo wa bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, usafi wa majengo na mpangilio wa bidhaa pamoja na kuangalia uwepo wa dawa zilizofutiwa usajili.

Kwa upande wake Afisa afya Mazingira wilayani Kibondo Bw.Joseph Kalobagwa amesema kuwa elimu huotolewa kila wanapotembelea maduka mbali mbali ili kuhimiza kuacha tabia ya kuagiza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Habari/Picha Na:-Kibondo Moto. 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad