TASWIRA:-Klabu ya Simba SC ilivyopitisha marekebisho ya Katiba mpya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 16, 2014

TASWIRA:-Klabu ya Simba SC ilivyopitisha marekebisho ya Katiba mpya.

Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Simba wakiwa kwenye mkutano wa marekebisho ya katiba Leo March 16,2014 na Mwenyekiti wa Simba SC, Ismail Aden Rage, akihutubia.…ambapo amesema kuwa marekebisho hayo yamefanyike kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika (CAF) na Tanzania (TFF).

Wanachama wa Simba SC wakiwa katika mkutano huo uliofanyika asubuhi ya leo March 16,2014,katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam.

Polisi wakiwa tayari kumkabili mmoja wa wanachama aliyetaka kuleta zogo kwenye mkutano huo.

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' akitoa hoja.

Rage akipongezwa na mmoja wawanachama wa Simba baada ya mkutano.

Wanachama wa Simba SC wakiwa katika mkutano huo uliofanyika asubuhi ya leo March 16,2014,katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam.

Rage na Kaburu wakikumbatiana baada ya mkutano.

Rage akipozi na Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Hassan Dalali.

Rage na Dalali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Simba SC.


WANACHAMA wa Simba SC leo March 16,2014, wamepitisha marekebisho ya Katiba yao katika mkutano uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar.

Mkutano huo ulijumuisha wanachama wote hai wa klabu hiyo pamoja na uongozi wa juu wa Simba wa Mwenyekiti, Ismael Aden Rage na kamati yake ya Utendaji.

Simba imefanya marekebisho kwenye ibara ya 26(5 )sifa za wagombea ambapo kipengele hicho awali kilikuwa kinasomeka “Asiwe aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kwa kuhukumiwa kifungo.

Kipengele hicho sasa kinasomeka “Asiwe ametiwa hatiani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita bila mbadala wa adhabu. Na endapo ametiwa hatihani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita, awe amemaliza muda wa miaka 5, tangu kuisha kwa kifungo husika bila kitiwa hatiana kwa jingine lolote la jinai.

Wanachama hao hao wamegoma kukipitisha ibara ya 26 (9) Mgombea awe ametimiza angalau miaka mitatu ya uanachama. Ambapo sasa kinasomeka angalau awe na mwaka mmoja wa wanachama.

Pia ibara ya 25 (8) (iii) wajumbe watano wa kamati ya utendaji. Mwenyekiti aruhusiwe kuteuwa wajumbe wengine watano wa kamati ya utendaji ambao anaweza kubadilisha kwa kadri anavyoona inafaa.

Wajumbe hawa wa kuteuliwa wanatakiwa kuwa na sifa zilizile wanazotakiwa kuwa nazo wajumbe wa kuchaguliwa na wanachama.

Baadhi ya vipengele vya katiba vilirekebishwa kwa kupigiwa kura na wanachama huku vingine kupitishwa moja kwa moja kulingana na hoja zilizokuwa zikitolewa mkutanoni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad