Mabingwa Watetezi wa, Ligi Kuu
Vodacom, Yanga SC, Leo March 26, 2014, hii Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
wameinyuka Tanzania Prisons Bao 5-0 .
Bao za Yanga SC zilifungwa na
Emmanuel Okwi, Dakika ya 20, Mrisho Ngasa, Dakika ya 37, na mbili za Hamisi
Kiiza, alieanzia Benchi na kufunga katika Dakika za 68 na 89, na Nadir Haroub
"Cannavaro" kufunga Bao moja kwa Penati ya Dakika ya 79.
Nao Prisons walipata Penati katika
Kipindi cha Kwanza baada ya Oscar Joshua kucheza Rafu lakini Mwangama alikosa.
Ushindi huo umewafanya Yanga
wafikishe Pointi 46 kwa Mechi 21 na wako Nafasi ya Pili nyuma ya Azam FC
waliocheza Mechi 22 na wana Pointi 50.
Mechi inayofuata kwa Yanga SC ni
Jumapili huko Mkwakwani dhidi ya Mgambo JKT.
Katika mechi nyingine ya Ligi kuu
ilikuwa ni Mgambo JKT dhidi ya Azam FC,ambapo bao za Kipindi cha Pili za John Bocco na Brian Umony zimewapa
ushindi wa Bao 2-0 Azam FC walipocheza na Mgambo JKT huko Mkwakwani Jijini
Tanga.
Matokeo haya yanawabakisha Azam FC
kileleni wakiwa Pointi 4 mbele ya Yanga lakini Yanga wana Mechi 1 pungufu.
Jumapili Azam FC wana kibarua kigumu
Jijini Dar es Salaam kwa kuivaa Simba SC.
VPL-LIGI KUU VODACOM 2013/2014.
Jumamosi Machi 29,2014.
Ashanti United v JKT Oljoro
Jumapili Machi 30,2014.
Mbeya City v Tanzania Prisons
Kagera Sugar v Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar v Coastal Union
JKT Ruvu v Rhino Rangers
Azam FC v Simba SC
Mgambo JKT
v Yanga SC
MSIMAMO.
| NA | TIMU | P | W | D | L | GD | PTS |
| 1 | Azam FC | 22 | 14 | 8 | 0 | 30 | 50 |
| 2 | Yanga SC | 21 | 13 | 7 | 1 | 27 | 46 |
| 3 | Mbeya City | 22 | 11 | 9 | 2 | 12 | 42 |
| 4 | Simba SC | 22 | 9 | 9 | 4 | 16 | 36 |
| 5 | Kagera Sugar | 21 | 8 | 8 | 5 | 3 | 32 |
| 6 | Coastal Union | 22 | 6 | 11 | 5 | 2 | 29 |
| 7 | Ruvu Shooting | 20 | 7 | 7 | 6 | -4 | 28 |
| 8 | Mtibwa Sugar | 21 | 6 | 8 | 7 | -1 | 26 |
| 9 | JKT Ruvu | 22 | 8 | 1 | 13 | -15 | 25 |
| 10 | Prisons FC | 21 | 3 | 10 | 8 | -9 | 19 |
| 11 | Ashanti United | 21 | 4 | 6 | 11 | -18 | 18 |
| 12 | Mgambo JKT | 21 | 4 | 6 | 11 | -19 | 18 |
| 13 | JKT Oljoro | 22 | 2 | 9 | 11 | -17 | 15 |
| 14 | Rhino Rangers | 22 | 2 | 7 | 13 | -17 | 13 |






No comments:
Post a Comment