Bao za Bayern katika Mechi hiyo ya Jana March 25, 2014,Usiku na Hertha
Berlin zilifungwa na Toni Kroos, Dakika ya 6, Mario Goetze, Dakika ya 14, na
Franck Ribery, Dakika ya 79 huku Bao la Hertha Berlin likifungwa kwa Penati ya
Dakika ya 66 iliyopigwa na Adrian Ramos.
Ubingwa huu ni wa tatu kwa Pep Guardiola katika msimu wake wa kwanza, alishinda UEF Super Cup mwaka jana mwezi August, kisha wakashinda ubingwa wa klabu bingwa ya dunia December mwaka jana.
Je Guardiola ataweka rekodi ya kubeba makombe manne ndani ya msimu wake wa kwanza na Bayern Munich kwa kuchukua ubingwa wa klabu bingwa ya ulaya?
Huu ni Msimu wa kwanza wa Kocha wao Pep Guardiola ambae hajafungwa hata
Mechi moja ya Bundesliga.
MSIMAMO-TIMU ZA JUU.
| NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
| 1 | Bayern Munich | 27 | 25 | 2 | 0 | 79 | 13 | 68 | 77 |
| 2 | BV Borussia Dortmund | 27 | 16 | 4 | 7 | 59 | 29 | 30 | 52 |
| 3 | Schalke 04 | 27 | 15 | 6 | 6 | 51 | 37 | 14 | 51 |
Katika Mechi nyingine iliyochezwa Jana Usiku , Timu zilizo Nafasi za
Pili na Tatu, Borussia Dortmund na Schalke 04 zilipambana na kutoka Sare
ya 0-0.
REKODI:
-Bayern
wamefunga si chini ya Bao 2 katika Mechi zao 18 zilizopita za Bundesliga,
ambazo zote wameshinda, na hizo zote ni Rekodi.
-Bayern
hawajafungwa katika Mechi 52 za Bundesliga na hii pia ni Rekodi.
BUNDESLIGA RATIBA/MATOKEO.
Jumanne Machi 25,2014.
BV Borussia Dortmund 0 Schalke 0
Hertha Berlin 1 Bayern Munich 3
SV Werder Bremen 1 VfL Wolfsburg 3
Eintr. Braunschweig 3 FSV Mainz 1
Jumatano Machi 26,2014.
Hamburger SV v SC Freiburg
FC Nuremberg v VfB Stuttgart
Eintracht Frankfurt v Borussia Mönchengladbach
TSG Hoffenheim v Hannover 96






No comments:
Post a Comment