Chelsea yapunguzwa kasi na Aston Villa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuchapwa bao 1-0 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 16, 2014

Chelsea yapunguzwa kasi na Aston Villa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuchapwa bao 1-0 .


Delph akipiga kichwa kumtungua kipa wa Chelsea,Petr Cech Uwanja wa Villa Park jana March 15,2014 na Chelsea kuchapwa bao 1-0 na Aston Villa Uwanja wa Villa park……..Matokeo hayo ya mchezo huo  yanaifanya Chelsea ibaki na pointi 66 baada ya kucheza mechi 30, ikiwa mbele ya Manchester City yenye pointi 60 baada ya mechi 27.


Meneja wa Chelsea Jose Mourinho akielekea jukwaani na alisirika na maamuzi ya mchezo na kutoa maneno yasiyofaa kitendo ambacho kilimfanya Refa Chris Foy amtoe nje.

Hapo Jana March 15,2014,Uwanja wa VILLA PARK, Chelsea, Vinara wa Ligi Kuu Uingereza, wamekiona cha moto baada kufungwa 1-0 na Aston Villa na pia kumaliza Gemu wakiwa Mtu 9 Uwanjani baada ya Kadi Nyekundu kwa Wachezaji wao wawili kutoka Brazil, Willian na Ramires, na pia Meneja wao Jose Mourinho kutolewa nje na Refa Chris Foy.

Balaa kwa Chelsea lilianza Dakika ya 69 baada ya Willian kumwangusha Mchezaji Bora wa Mechi hii, Fabian Delph, na kulambwa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Katika Dakika ya 82, Delph alikokota Mpira na kuwatambuka Wachezaji kadhaa wa Chelsea na kumpasia kwenye Winga Mark Albrighton ambae alitoa krosi ya chini iliyochezwa kwa kisigino na Delph na kufunga Bao zuri na la ajabu.

Huku Dakika zikiyoyoma, Ramires wa Chelsea alipewa Kadi Nyekundu kwa kumkita El Ahmadi na tukio hilo lilimfanya Meneja wa Chelsea Jose Mourinho akasirike na kutoa maneno yasiyofaa kitendo ambacho kilimfanya Refa Chris Foy amtoe nje.

Chelsea bado imebaki kileleni ikiwa Pointi 6 mbele ya Man City lakini wao wamecheza Mechi 3 zaidi ya Man City.

Matokeo ya EPL 2013,2014 ,Jumamosi Machi 15,2014.

Hull 0 Man City 2
Everton 2 Cardiff 1
Fulham 1 Newcastle 0
Southampton 4 Norwich 2
Stoke 3 West Ham 1
Sunderland 0 Crystal Palace 0
Swansea 1 West Brom 2
Aston Villa 1 Chelsea 0


Ratiba ya Ligi kuu soka Uingereza (EPL) 2013,2014.

Jumapili Machi 16,2014.

1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad