Taswira ya Utekaji wa magari katika kijiji cha Kisaki mkoani Singida. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 04, 2014

Taswira ya Utekaji wa magari katika kijiji cha Kisaki mkoani Singida.

Baadhi ya magari yaliyokwama kupita baada ya kufanyika kwa utekaji wa magari katika eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida,ambapo Dereva wa lori lililotekwa,Bw.Agustino Mbawala, akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida , amesema aliona mawe makubwa barabarani na kuamua kusimama na kukimbia lakini wali mvamia na kumpiga hatimaye  kumpora fedha na simu.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP.Geofrey Kamwela, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya tukio la utekaji wa magari katika eneo la Kisaki manispaa ya Singida. Naibu Waziri wa Afrika Mashariki Abdula J. Abdula ametoa wito kwa madereva kuacha mara moja vitendo vya kuziba barabara kwa madai ya kudai haki zao kuwa vinachangia kusababisha madhara mengi.
Madereva hao wa malori zaidi ya mia tatu waligoma kuendelea na safari katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao aliyekuwa akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki manispaa ya Singida.
Baadhi ya magari yaliyokwama kupita baada ya kufanyika kwa utekaji wa magari katika eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.

Wakiongea na waandishi wa habari, madereva ambao wamekutwa katika eneo hilo wameomba  jeshi la polisi kufanya doria mara kwa mara eneo hilo kwani kumekuwa na matuki  yanayo jirudia ya utekeji wa magari  kwa kuweka mawe makubwa barabarani na kuwajeruhi madereva jambo ambalo lina tishia amani kwa watumiaji wa barabara.

Madereva wa malori baada ya kufunga barabara naibu waziri wa Afrika mashariki Dr. Abdulla Abdulla alikumbwa na adha hiyo na kusema ni haki ya kikatiba kwa madereva kugoma kwa kudai haki zao, kutokana na hali hiyo amewahaidi madereva kupeleka kilio chao katika mamlaka husika ili kuweza kutatua tatizo lao na kukomesha vitendo vya uvamizi wa magari katika eneo hilo.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida  SACP Geofrey Kamwela amesema madereva waliamua kusimama barabarani bila sababu yeyote kwa muda wa zaidi ya masaa matatu na kusababisha foleni kubwa ambapo kwamujibu wa sheria za usalama barabarani walikuwa wamefanya kosa ,lakini baada ya viongozi kufika na kuwasikiliza waliamua kuendelea na safari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad